29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

ALGERIA YATUPWA NJE KUFUZU KOMBE LA DUNIA

CONSTANTINE, ALGERIA

HATIMAYE timu ya Taifa ya Algeria imezima ndoto zake za kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi baada ya juzi kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Zambia ‘Chipolopolo’

Mchezo huo wa kuwania kufuzu ulipigwa kwenye Uwanja wa Mohamed-Hamlaoui mjini Constantine nchini Algeria, wenyeji walishindwa kutamba kwenye uwanja wa nyumbani unaochukua jumla ya watazamaji 45,000.

Mchezo wa awali ambao ulipigwa nchini Zambia, wenyeji walifanikiwa kushinda mabao 3-1, hivyo mchezo wa juzi walikuwa na kazi rahisi kuweza kufanya vizuri.

Kutokana na hali hiyo, Algeria wanaungana na Cameroon ambao walikuwa wa kwanza kwa Afrika kuondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Nigeria.

Kwa upande mwingine timu ya Taifa ya Tunisia na Misri zimeanza kujihakikishia kufuzu Kombe la Dunia baada ya kufanya vizuri kwenye michezo yao.

Tunisia wao wanaongoza katika msimamo kwenye kundi la A, huku wakiwa na pointi 10 wakifuatiwa na DR Congo wenye pointi 7 baada ya wote kucheza michezo minne, wakati huo Misri wakiwa wanaongoza kwenye kundi lao E, wakiwa na pointi tisa wakifuatiwa na Uganda wenye pointi saba.

Misri wao wanataka kuandika historia mpya ya kufuzu katika hatua hiyo kama walivyofanya mwaka 1990 baada ya mchezo wa juzi kushinda bao 1-0 dhidi ya Uganda. Wiki iliyopita Misri walipoteza mchezo wao kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Uganda, mchezo uliopigwa mjini Kampala, lakini juzi wakalipiza kisasi huku bao pekee likifungwa na mshambuliaji wao, Mohamed Salah, wakati lile la nchini Uganda likifungwa na Emmanuel Okwi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles