24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MBARONI KWA KUMBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI

Na JUDITH NYANGE – MWANZA

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Samweli Masumbuko (32), Mkazi wa Kata ya Mahina wilayani Nyamagana, kwa tuhuma za kumbaka  mwanafunzi wa darasa la pili (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 10.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,  Ahmed Msangi, mtuhumiwa huyo alikamatwa Aprili 1, mwaka huu saa 11:00 jioni katika Mtaa wa Mwembeni, Kata ya Mahina.

Kamanda Msangi alisema mtuhumiwa anadaiwa kuwa alimbaka mwanafunzi huyo Machi 25, mwaka huu saa 11:00 jioni, lakini kwa kipindi chote hicho hakuweza kusema kwa mtu yeyote hadi Aprili 1, mwaka huu mama  yake alipogundua mwanawe kufanyiwa ukatili huo.

“Mama wa mtoto huyo aligundua tukio la kubakwa kwa mwanawe wakati akimwogesha, kisha akatoa taarifa polisi ambao walifanya ufuatiliaji wa haraka kwa kushirikiana na wananchi na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.

“Samweli Masumbuko anakabiliwa na tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Mahina na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri,” alisema Kamanda Msangi.

Alisema upelelezi dhidi ya watu waliohusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha au kushawishi ukatili huo bado unaendelea na kwamba mtuhumiwa anahojiwa na Jeshi la Polisi na pindi uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Hata hivyo, Kamanda Msangi amewashauri wazazi au walezi kuwa na utaratibu wa kuwakagua watoto wao mara kwa mara ili kuweza kubaini mapema kama wana tatizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles