24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAOMBWA KUWAWEZESHA WENYE VITUO VYA USONJI

Meneja Masoko na Utafiti kutoka Kampuni ya Maxicom, Deogratius Mosha
Na Gabriel Mushi – Dar es Salaam

SERIKALI imetakiwa kuweka mazingira rafiki kwa watu wanaotaka kuanzisha vituo vya kuwalea watoto wanaokabiliwa na tatizo la usonji ili kuongeza uelewa dhidi ya tatizo hilo nchini.

Wito huo ulitolewa juzi Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kituo cha kulea watoto wenye usonji, Kunduchi, Shaban Omar, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matembezi maalumu ya kujenga uelewa dhidi ya ugonjwa huo nchini.

Alisema Tanzania bado ina changamoto ya uelewa dhidi ya ugonjwa wa usonji jambo linalochangia wengi kutoutibu kutokana na kutoelewa dalili zake.

“Alisema usonji ni hali ya udhaifu katika ukuaji wa ubongo, ambayo huleta athari kubwa katika mawasiliano, mahusiano ya kijamii na utambuzi. Tatizo hili ni la dunia nzima na bado hakuna maelekezo kamili ya chanzo chake wala tiba.

“Dalili za usonji bado hazijafahamika vizuri kwa wazazi na walimu nchini, hivyo wanashindwa kuutibu ugonjwa huu au kupata msaada wa kitaalamu kwani ni ugonjwa ambao una mambo mengi yanayoathiri namna mtu anavyowasiliana, na mara nyingi huwa na tabia ya kufanya vitu kwa kurudia rudia bila kukusudia,” alisema Omar.

Aidha, Meneja Masoko na Utafiti kutoka Kampuni ya Maxicom, Deogratius Mosha, alisema watashirikiana na kituo hicho kwa kutumia teknolojia ya ICT kusambaza ujumbe ili kujenga uelewa kuhusu tatizo la usonji.

“Pia nitoe wito kwa wazazi wenye watoto ambao wana tatizo la usonji nchini kuwapenda, kuwatunza na kuwapa mahitaji yao kama watoto wengine kwani ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu kuwapa watoto hao,” alisema.

Naye Balozi wa kituo hicho kinachofahamika kwa jina la Autism Therapy & Behaviopur Learning Centre, Emanuel Likuda, alisema Serikali inatakiwa kupunguza urasimu katika usajili wa vituo vya ina hiyo pamoja na kutoa kodi katika uingizaji wa vifaa tiba kwa watu wenye tatizo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles