24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Mbaroni akidaiwa kumuua mama yake, akutwa akinywa damu kwenye kikombe

Na JANETH MUSHI -ARUSHA

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha, linamshikilia Daniel Emanuel(32), mkazi wa Sakila wilayani Arumeru kwa tuhuma za kumuua  mama yake mzazi, Eliyamulika Sarakikya(79), kwa kumkata na shoka kisha kunywa damu yake.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kukinga damu ya mama yake ambapo alikutwa akiinywa katika kikombe baada ya kumuua kwa  kumkata na shoka kisha kumtenganisha shingo, mkono, mguu na kiwiliwili.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Jonathan Shanna, alisema mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Mei 15 mwaka huu saa tisa mchana katika Kijiji cha Sakila chini, Kata ya Kikatiti,Tarafa ya King’ori wilayani Arumeru.

“Mtuhumiwa alimkata kwa shoka shingoni mama yake na kutenganisha na mwili wale na akaona haitoshi akakata mguu wa kulia na kuutenganisha na akakata mguu wa kushoto  pia akautenganisha wakati anafanya unyama huu alikuwa anakinga damu kwenye kikombe anakunywa,”alisema

Alisema wakati akifanya tukio hilo majirani walishuhudia akinywa damu na kwamba polisi walipofika eneo la tukio mtuhumiwa alitupa kikombe alichokuwa ameshika mkononi kikiwa kimetapaa damu na kujaribu kukimbia.

“Lakini tulifanikiwa kumkamata na tumemweka mahabusu hadi upelelezi utakapokamilika, ila katika hatua za awali za uchunguzi inadaiwa mtuhumiwa ana matatizo ya akili,tunafuatilia hilo pia,”alisema

“Lakini hili sikubaliani sana sababu aliwezaje kuandaa shoka, mazingira tulivu yasio na watu, pia kwanini kama hana akili alikimbia polisi alipowaona na alipokamatwa alikataa kuhojiwa na Polisi, hili linanipa shaka,”

Alisema kutokana na tukio hilo amemuagiza askari wa upelelezi wa kesi hiyo kuwasiliana na madaktari ili kumpima kama mtuhumiwa huyo ana matatizo ya akili kama inavyodaiwa.

“Nitoe wito kwa wananchi wote wanaoishi na ndugu, jamaa au marafiki ambao wana matatizo ya akili kuwapeleka katika hospitali maalumu ambazo zipo kwa ajili ya kutibu watu wenye matatizo 

kama hayo ili kuepusha madhara ambayo wanaweza kusababishwa katika jamii,”aliongeza.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,310FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles