27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WATU 11 WAFARIKI DUNIA MOROGORO

Na Ashura Kazinja – MOROGORO

WATU 11 wamefariki dunia mkoani Morogoro kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba na wengine kusombwa na maji, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Akithibitisha vifo hivyo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroard Mutafungwa, alisema watu wanne wa familia moja

walifariki dunia kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba walipokuwa wamelala huku wengine saba wakisombwa na maji ya mvua.

Kamanda Mutafungwa alisema tukio la kwanza lilitokea Mei 15 saa 7 usiku, katika maeneo ya Kijiji cha Konde  tarafa ya Matombo Wilaya ya Mkoa wa Morogoro, ambapo watu wanne wa familia moja walifariki dunia kwa kudondokewa na ukuta wa nyumba yao wakiwa

wamelala kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Aliwataja marehemu hao kuwa ni Godfrey Augustin (35), Joyce Claud (38), Mariana Godfrey (10) mwanafunzi wa Shule ya Msingi Konde na

Senorino Godfrey (5) wote wakazi wa kijiji cha Konde.

Alisema watu wengine saba wakiwemo watoto watano walifariki dunia kwa

kusombwa na maji yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha maeneo ya milimani na kusababisha maji mengi kuporomoka na kuingia

kwenye nyumba zao wakati wamelala usiku wa saa 8, huko katika kijiji

na kata ya Pemba tarafa na Wilaya ya Mvomero mkoani hapa.

Mutafungwa alisema watu hao waliofariki ni Peter Ferdnand (66),  Tumbo John (37), Kauva Peter (35),  Jack Tumbo (6), Kadudu Fikiri (9), Madi

Fikiri (14) na Mtupe John (8), wote wakiwa ni wakazi wa kijiji cha Pemba.

Aidha Mtafungwa alisema kuwa katika tukio hilo mtoto mchanga wa kiume wa marehemu Kauva Peter ambaye alikuwa bado hajapewa jina naye anahisiwa kufariki dunia, na kwamba mwili wake bado haujapatikana na

juhudi za kuutafuta bado zinaendelea.

Mutafungwa alisema miili ya Marehemu tayari imeshafanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya taratibu za

Mazishi.

Kamanda huyo pia  aliwataka    wananchi kuwa na tahadhari na mvua zinazoendelea kunyesha kwa kuepuka kuishi maeneo yaliyo karibu na njia za maji na kwenye nyumba za udongo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles