Mayanga: Bado nina kazi kubwa

0
843

salum-mayangaNa THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar, Salum Mayanga, amesema bado ana kazi kubwa kukinoa kikosi chake ili kiendelee kufanya vizuri kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo uliopita Mtibwa walitoshana nguvu na Mbao FC, baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye uwanja wao wa Manungu uliopo Morogoro.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mayanga alisema hakuna timu ya kubeza msimu huu kwani kila mtu anaonekana kuwa makini na kuhitaji pointi tatu muhimu.

“Ligi ni ngumu msimu huu na kila timu inashinda sehemu yoyote pale hakuna ugenini, hivyo nitahakikisha nawajenga wachezaji wangu ili wazidi kuimarika na kufanya vizuri kwa kila mchezo,” alisema.

Alisema baada ya kutoka sare na Mbao, kwa sasa anajiandaa kwa mchezo unaofuata dhidi ya African Lyon, unaotarajiwa kupigwa Jumapili kwenye uwanja huo.

Mayanga alisema kupitia mchezo uliopita aliyasoma makosa yaliyopo kwenye kikosi chake na anaenda kuyafanyia kazi ili yasijitokeze kwa mara nyingine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here