30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TAMWA: Sheria za barabarani zirekebishwe kusaidia wanawake,watoto

Mkurugenzi Mtendaji Edda Sanga
Mkurugenzi Mtendaji Edda Sanga

Chama cha Wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA) kimewaasa wadau wa usalama barabarani kuzifanyia marekebisho sheria na kanuni zake ili ziwalinde wanawake na watoto.

TAMWA imesisitiza kuwa maeneo ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika marekebisho ni mwendo kasi,  ulevi wakati wa uendeshaji, uvaaji kofia ngumu, kufunga mikanda na vizuizi kwa watoto.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, kuanzia Januari hadi Julai,2016,  watu 1580 wamekufa kutokana na ajali barabarani, wengine 4659 walijeruhiwa katika ajali  5152 zilizotokea nchi nzima.

Na takwimu za shirika la Afya Duniani (WHO) Watu milioni 1.25 hufariki kila mwaka kwa ajali za barabarani.

Mkurugenzi Mtendaji TAMWA, Edda Sanga alisema, “Ukweli ni kwamba wanawake na watoto ndio wanaoathirika zaidi kwani watoto hukosa huduma na mahitaji  ya msingi baada ya kupoteza watu wanaowategemea,”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles