28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Mawakili wajitoa kesi ya Kova, Nzowa

Na JANETH MUSHI-ARUSHA

MAHAKAMA ya Rufaa ya Tanzania imeshindwa kusikiliza shauri la kugombea nyumba kati ya aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini, Kamishna Godfrey Nzowa na Kamanda mstaafu wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.

Kesi hiyo iliyokuwa isikilizwe jana, ilikwama kusikilizwa baada ya mawakili wa Nzowa kujitoa kwa sababu ya kutokuwa na maelezo sahihi na ya kutosha kutoka kwa mteja wao – mleta maombi juu ya shauri hilo.

Shauri hilo la madai kati ya maofisa hao wawili waandamizi wa Jeshi la Polisi wanagombea nyumba ya Serikali iliyopo eneo la Uzunguni, jijini Arusha linasikilizwa na Jaji Sivangilwa Mwangesi.

Mawakili hao waliojitoa ni Modest Akida na Neema Mtayangulwa.

“Hatukupewa maelezo ya kutosha na mleta maombi, hivyo huwezi kumtetea mtu ambaye hajakupa maelezo ya kutosha,” alidai Wakili Akida.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Mwangesi aliahirisha rufaa hiyo hadi siku nyingine itakayopangwa.

Nyumba inayogombewa na wawili hao ni kati ya nyumba walizokuwa wakiishi watumishi wa umma wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, kabla hazijauzwa kwa wafanyakazi.

Nzowa anapinga Kova na wenzake kuuziwa nyumba hiyo ambayo awali alikuwa akiishi wakati alipokuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO), Mkoa wa Arusha.

Nyumba hiyo aliuziwa Kamishna Kova wakati akiwa tayari amehama mkoani hapa na wakati inauzwa, Nzowa alikuwa bado ni RCO Arusha na alikuwa akiishi ndani ya nyumba hiyo na familia yake kabla ya kuhamishiwa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles