24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mavunde awataka walimu wanawake kuchangamkia fursa za kiuchumi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amewataka walimu wanawake jijini Dodoma kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo ili kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi.

Mavunde amesema hayo jana katika hafla ya Walimu Wanawake wa Dodoma (Dodoma Women Teachers Gala) ambapo pamoja na mambo mengine amewataka walimu hao kuitumia fursa ya ukuaji wa uchumi wa Jiji la Dodoma kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kutumia mikopo ya aslimia nne ya mapato ya ndani ya jiji na kampuni za ukopeshaji mashine na mitambo mbalimbali.

“Nawapongeza waandaji wa hafla hii ambayo imewakutanisha walimu wanawake kutoka maeneo mbalimbali kuja kujadiliana fursa za kiuchumi na kumkomboa mwalimu mwanamke kiuchumi.

“Mwakani hafla hii tutaifanya kubwa zaidi na kuongeza idadi ya walimu washiriki na taasisi za kuwajengea uwezo. Nimefurahi kuona bidhaa za ujasiriamali unaofanywa na walimu, niwaombe walimu wengi zaidi mchangamkie fursa hii iliyopo Dodoma kwa sasa kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kujiongezea kipato na mimi nipo tayari kuwaunga mkono kufikia malengo yenu hayo,” amesema Mavunde.

Awali, Mwenyekiti wa Wote Forum, Mwalimu Sheila Chinja amewashukuru walimu wote kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika hafla hiyo na kuahidi kuiboresha zaidi mwakani ili kuongeza tija katika ukombozi wa kiuchumi wa mwalimu mwanamke.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Neema Majule na wazungumzaji maarufu nchini, Aunt Sadaka na Irene Mbowe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles