27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Mavunde ashiriki ujenzi wa zahanati

MWANDISHI WETU-DODOMA

MBUNGE wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde (CCM), ameshiriki hatua za awali za ujenzi wa Zahanati ya Mtaa wa Msembeta, Kata ya Chigongwe jijini Dodoma.

Mavunde ameshiriki ujenzi huo juzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake kwa wananchi hao aliyoitoa Aprili 6, mwaka huu, wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi ambapo hoja ya ukosefu wa zahanati ilijitokeza na Mbunge Mavunde akaahidi kuanzisha ujenzi wake.

Pamoja na Mavunde kushiriki kuchimba msingi wa zahanati hiyo akishirikiana na wananchi, pia alikabidhi mifuko 100 ya saruji na kuahidi kusimamia kukamilika kwa zahanati hiyo na kuondoa adha ya wakazi wa kata hiyo ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya katika maeneo jirani.

Pamoja na hayo, Mavunde aliwataka wakazi wa kata hiyo kuendelea kushirikiana na viongozi wao ili waweze kurahisisha upatikanaji wa maendeleo katika maeneo yao.

“Ninawapongeza wananchi kwa kujitolea baadhi ya vifaa vya ujenzi na nguvu kazi ili kukamilisha ujenzi huu.

“Kwa upande wangu, nataka niwaahidi kwamba, nitahakikisha zahanati hii inakamilika ili kuondoa adha hii kwa wananchi.

“Pia, nitashirikisha makampuni ya madini yaliyopo katika kata hii ili nayo yaunge mkono jitihada hizi za wananchi na mimi mbunge katika kukamilisha ujenzi huu kwani kukamilika kwa zahanati hii, kitakuwa ni kichocheo cha maendeleo katika kata yetu,” alisema.

Akishukuru kwa niaba ya wananchi wenzake, mmoja wa wananchi wa kata hiyo, Esther Masimami, alimshukuru Mbunge Mavunde kwa kuanzisha mchakato huo wa ujenzi wa zahanati ambao alisema utawapunguzia kero ya ukosefu wa huduma za afya.

“Pia, nakupongeza kwa jinsi ulivyoahidi kujitolea katika nguvu kazi kama sehemu ya mchango wako wa ujenzi wa zahanati yetu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles