22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mavugo sina mkataba Vital’O

Laudit-MavugoNa ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI mahiri wa timu ya Simba, Laudit Mavugo, amekana kuwa na mkataba na klabu yake ya zamani ya Vital’O ya Burundi, akieleza kwamba yeye ni mchezaji huru.

Mavugo ametoa kauli hiyo baada ya jana kuzuka taarifa kuwa klabu yake hiyo ya zamani imedai kuwa na mkataba naye wa mwaka mmoja na imetuma jina lake Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kama mmoja wa wachezaji watakaokuwa nao.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mavugo alisema kwamba alifikia uamuzi wa kujiunga na Simba baada ya kuhakikisha kwamba amemaliza mkataba na timu yake ya Vital’O, hivyo haoni kitakachomsumbua.

“Mashabiki wasiwe na wasiwasi kwani nilijiunga na timu ya Simba nikiwa mchezaji huru, sina mkataba na yeyote na kama watafanya hivyo basi ni kwa maamuzi yao wenyewe,” alisema Mavugo.

Hata hivyo, MTANZANIA lilijaribu kutafuta ukweli wa suala hili ndani ya klabu ya Simba, ambapo lilielezwa kuwa   wametuma majina ya wachezaji waliowasajili katika Mtandao wa Usajili wa Kimataifa (TMS), ambao kumbukumbu zake hutunzwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), hivyo Shirikisho hilo ndilo litaeleza kama Mavugo ana mkataba Vital’O au la.

“Watu wa Simba wasitishwe sana na suala hili, tumetuma majina na baada ya wiki mbili tutajua kama kweli alikuwa  mchezaji huru au alitudanganya kwa kuwa wakati huo Fifa watakuwa wakitoa hati za uamisho kwa wachezaji wapya (ITC).

“Tumemalizana na mchezaji binafsi kuhusu mkataba, bado tunafuatilia ukweli kuhusu madai ya klabu yake, yote yanawezekana kutatuliwa,” kilisema chanzo hicho ambacho kilikataa kutajwa jina lake.

Awali kabla ya ujio wa nyota huyo wa Burundi katika timu ya Simba, Rais wa Simba, Evans Aveva, alinukuliwa akisema kwamba  walikosa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa Vital’O ili wazungumzie suala la mkataba wa Mavugo.

Hata hivyo, Aveva alisema dhamira yao ni kumsajili Mavugo na wangeendelea na jitihada kuhakikisha wanafanikiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles