23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mufti Zubery aunda tume kuchunguza ufisadi Bakwata

SHEIKH A ZUBERINa Veronica Romwald, Dar es Salaam

MUFTI Mkuu wa Tanzania , Sheikh Abubakar Zubeiry ameunda tume ya wajumbe wanane na kuipa majukumu makuu sita, ikiwamo kufuatilia mikataba yote ya uuzaji wa viwanja na mali mbalimbali za baraza na taasisi zake nchi zima sambamba na kuona uhalali wa umiliki huo.

Tume hiyo ameiunda kwa mujibu wa Katiba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kipengele 82 (3) b.

Taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Bakwata, ilieleza kuwa Mufti Zubeiry,  alisema tume hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Sheikh Abuubakar Khalid.

“Pamoja na Sheikh Khalid wajumbe wengine ni Sheikh Issa Othman ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti, Mwalimu Salim Abeid (Katibu) na wajumbe ni Sheikh Khamis Mataka, Ustaadh Tabu Kawambwa, Mwalimu Ally Abdallah, Alhaj Omar Igge na Sheikh Mohamed Khamis,” alisema.

Alisema mbali na kufuatilia mikataba, tume hiyo imepewa jukumu la kufuatilia suala la misamaha ya kodi mbalimbali zilizoombwa na baraza na taasisi zake nchi zima.

“Itafuatilia mikataba yote ambayo baraza na taasisi zake nchi zima, zimeingia na wawekezaji na kuona mikataba hiyo kama ina masilahi na baraza au kinyume na hivyo,” alisema.

Alisema pia itafuatilia mikataba yote ambayo Bakwata na taasisi zake nchi zima, zimeingia na wapangaji mbalimbali katika maeneo yanayomilikiwa na baraza na taasisi zake.

Mufti huyo alisema tume hiyo itafuatilia mali zote za baraza nchi nzima na kuona hali ya usajili wa mali hizo.

“Itafuatilia pia mapato na matumizi ya Baraza na taasisi zake nchi nzima. Na italeta taarifa na mapendekezo  yake ofisini  ndani ya siku 60 kuanzia leo (jana),” alisema.

Juni 6, mwaka huu akihutubia katika Baraza la Eid El Fitri Rais Dk. John Magufuli alitangaza vita dhidi ya viongozi wa Serikali na wawekezaji wanaofanya dhuluma na kuchukua mali za madhehebu ya dini nchini.

Alisema viongozi hao wamekuwa wakiwahadaa viongozi wa dini na kisha kuingia nao mkataba ya kitapeli na baadaye wanadhulumu mali za taasisi za dini.

“Nakumbuka nilipokuwa Waziri wa Ardhi viongozi wa Bakwata mlikuwa mnakuja ofisini kwangu kulalamika juu ya suala hili, wanawadanganya mnaingia nao ubia kumbe ni wa kitapeli.

“Nawashauri Bakwata kuwatumia mawakili mlionaona pamoja na viongozi wa madhehebu mengine kuhakikisha mnakomboa mali za taasisi zenu ili zisije zikasababisha migogoro itakayoleta uvunjifu wa amani,” alisema

Rais Magufuli aliahidi kwamba Serikali yake itashirikiana na viongozi wa dini katika kuzikomboa mali zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles