23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

MATIBABU YA KIFAFA CHA MIMBA

Dr. Imani Kondo, Czech

Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye mimba za kwanza.

Kwa walio wengi, ugonjwa huu hutokana na kupanda kwa msukumo wa damu (High blood pressure). Ugonjwa huu utokeapo, mgonjwa hupatwa na degedege (convulsions).

Kifafa cha uzazi au wengine wanakiita kifafa cha mimba ni miongoni mwa matatizo yanayosababisha vifo vya wajawazito nchini.

Kifafa cha mimba kinaweza kutokea wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au baada
ya kujifungua

Matibabu ya kifafa cha mimba

Tiba pekee ya kifafa cha mimba ni kumzalisha mjamzito. Hii ni kwa sababu ugonjwa huu husababishwa na kuwepo kwa kondo la nyumba ndani ya kifuko cha uzazi. Bila kutoa kondo la nyuma mgonjwa hawezi kupona.

Iwapo ugonjwa huu utagundulika kabla mtoto hajakomaa na kuwa tayari kwa kuzalishwa.

Daktari anaweza kushauri mjamzito alazwe na kuangaliwa kwa ukaribu wakati ikisubiriwa kukomaa kwa mtoto. Vilevile daktari anaweza kushauri mjamzito apewe dawa ya kuharakisha kukomaa mapafu ya mtoto.

Iwapo hali ya mjamzito ikibadilika na kuwa mbaya, kumzalisha itakuwa ni lazima hata kama mtoto hajakomaa kwa sababu kuna hatari kubwa ya mama na mtoto kuathirika iwapo ujauzito utaendelea kuwepo.

Mojawapo ya hatari inayoweza kutokea iwapo ujauzito utaachwa ni mtoto kufia tumboni, kupoteza fahamu kwa mjamzito na kupata dalili za “degedege“.

Pia mgonjwa anaweza  kupoteza uwezo wa damu pamoja  kuganda jambo ambalo  husababisha  mjamzito kupoteza damu nyingi.

 Damu inapoganda  mwilini na kuziba mishipa, kondo la nyuma hujitenga na kifuko cha uzazi kabla ya mtoto kuzaliwa  pia  figo za mjamzito hushindwa kabisa kufanya kazi, mjamzito kupata kiharusi (stroke) au kupoteza maisha kabisa.

Kwenye kumzalisha mama mwenye kifafa cha mimba njia mbalimbali huweza kutumika kutegemeana na hali ya mjamzito.

Itaendelea wiki ijayo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles