23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

MAALIM SEIF: LEMA NI KIONGOZI SHUJAA

Na Janeth Mushi, Arusha

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),  Maalim Seif Sharif Hamad amesema amefurahi kumuona Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) akiwa na afya njema na kusisitiza kuwa ni kiongozi shujaa. 

Maalim Seif aliyasema hayo leo nje ya Gereza Kuu la Kisongo, Arusha baada yakuongea na Lema ambaye anashikiliwa mahabusu gerezani hapo.

Aliongeza kuwa kiongozi huyo akitoka gerezani atakuwa ngangari na mwenye ushujaa zaidi na kuwa waliomuweka gerezani wakidhani atavunjika moyo na kuogopa,hawataweza.

"Lema akitoka atakuwa ngangari zaidi kuliko sasa hivi na bado ataendelea na mapambano haya na yumo katika hali ya kishujaa,ushujaa wake umeongezeka na nimepata moyo kuwa yuko katika hali nzuri kiafya na anasubiri uamuzi wa mahakama," alisema Maalim Seif.

Akizungumzia hali ya mgogoro ndani ya Chama hicho,alidai kuwa mgogoro uliopo ndani ya chama hicho siyo kati yake na aliyekuwa Mwenyekiti  wa CUF Taifa,Profesa Ibrahim Lipumba na kuwa yeye binafsi hana tatizo na Lipumba na kuwa CUF ni chama kimoja ila  Lipumba na genge lake ni waasi wa chama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles