24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Maskini Boris, hana jema Brexit!

LONDON, UINGEREZA

KIONGOZI wa chama cha upinzani nchini Uingereza Jeremy Corbyn amesema atawaamuru wabunge wa chama chake wayapinge mapendekezo mapya juu Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Boris Johnson.

 Corbyn amesema mapendekezo hayo hayazingatii hali halisi na yataleta madhara.

Corbyn ameeleza kuwa hata Waziri Mkuu mwenyewe anatambua kwamba mapendekezo hayo yatapingwa na Umoja wa Ulaya lakini Waziri Mkuu Boris amepinga madai hayo na ameeleza kuwa serikali yake imefanya juhudi za dhati kuondosha mkwamo katika mchakato wa Brexit huku muda ukiyoyoma kufikia mwishoni mwa mwezi huu ambapo Uingereza inatarajia kujiondoa Umoja wa Ulaya.

Wakati huo huo Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Donald Tusk ameandika kwenye Twitter kuwa Jumuiya hiyo inasimama thabiti na Jamuhuri ya Ireland lakini pia amesema Umoja huo haujaridhishwa na mapendekezo mapya ya Boris.

WABUNGE WAUSASAMBUA Juzi baada ya mpango huo  mpya kuwasilishwa bungeni  ulikosolewa wabunge kutoka vyama takriban vyote nchini Uingereza baada ya Umoja wa Ulaya pia kuonesha kutoridhishwa kabisa na mpango huo.

Boris  aliwasilisha mapendekezo yake mapya kuhusu Brexit, siku moja baada ya kuyawasilisha mapendekezo hayo mbele ya viongozi wa Umoja wa Ulaya.

Mapendekezo hayo yameibua mabishano makali ndani ya Bunge la Uingereza.

Kundi muhimu la wabunge wa Umoja wa Ulaya limesema bunge la Ulaya halikuweza kuunga mkono makubaliano kwa kuzingatia mapendekezo hayo mapya ya Uingereza ambayo hayajafikia vigezo vinavyotakiwa kuhusu suala la mpaka.

Ndani ya bunge la Uingereza kiongozi wa chama kinachotawala Scotland cha SNP, Ian Blackford amesema mapendekezo ya sasa ya waziri mkuu Boris Johnson hayakubaliki mbele ya Wascotland.

” Mapendekezo haya hayakubaliki, hayawezi kufanyiwa kazi, hayawezi kupendekezwa. Yanahusu tu kumbebesha lawama mtu mwingine, na kwa maana hii katika Umoja wa Ulaya mpango huu umekataliwa.

“Spika mpango huu umetengenezwa kushindwa na hilo analijuwa waziri mkuu. Hiki kitiisho cha kuwataka watu waukubali au wauachilie mbali ni shinikizo jingine linalotueleza kwenye hatua ya kuondoka Umoja wa Ulaya kwa janga kubwa.”

Ian Blackford pia amesema wabunge wa Scotland wako tayari kuiangusha serikali ya Boris Johnson ikiwa waziri mkuu huyo atashikilia msimamo wa kulazimisha Brexit bila makubaliano.

”Namwambia waziri mkuu, tafuta njia urefushe muda wa Brexit  au ujiuzulu, la sivvyo SNP iko tayari kuiangusha serikali hii.”

Kwa upande wake Corbyn alisema hakuna mbunge yoyote wa chama chake atakayeunga mkono mapendekezo  hayo mapya ambayo amesema hayana tafauti na yale yaliyokataliwa huko nyuma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles