24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Baada ya Ukraine,Trump aiomba China imchunguze Joe Biden

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani, Donald Trump ambaye tayari anakabiliwa na shutuma inayoweza kumwondoa madarakani baada ya kumtaka rais wa Ukraine kumchunguza mpinzani wake Joe Biden, na sasa inaelezwa kuwa aliwatakata China wafanye vivyo hivyo.

Aliziambia nchi zote mbili, China na Ukraine kumchunguza Biden ambaye ni kinara wa chama cha Democratic anayetaka kuwania urais, na mtoto wake.

Hayo yamejiri siku chache baada ya mazungumzo ya siri ya simu ya Trump yanayotajwa kuwa na nia ya kumsambaratisha mpinzani wake kisiasa, Biden kunaswa, na Ofisa wa Shirika la Kijasusi la CIA.

Democrat imemshutumu Rais Trump kwa madai ya kutoa msaada wa kijeshi kama njia ya kumfanya aweze kuibua mabaya ya Biden.

Biden alijibu kupitia ukurasa wake wa tweeter kuwa ni utani Trump ana wazo la kumshambulia mtu yeyote mwenye msimamo.

Mazungumzo ya simu kati ya rais Trump na kiongozi wa Ukraine Rais Volodymyr Zelensky,Julai 25 yalisababisha wapelelezi kupeleka taarifa zinazoweza kumuondoa Trump madarakani.

Ingawa siku ya alhamisi, rais Trump alidai kuwa madai hayo ni upuuzi.

Katika ujumbe wake wa usiku wa manane kupitia kurasa yake ya Tweeter, Trump aliongeza kuwa yeye ana jukumu la kuchunguza kashfa za rushwa, jambo ambalo linajumuisha na kuuliza na kutoa mapendekezo kwa nchi jirani kutoa msaada.

Trump anamshutumu Biden na mtoto wake Hunter kwa kashfa za rushwa katika mikataba yao ya kibiashara na kisiasa nchini Ukraine na China,

Hadi sasa Trump hajatoa ushahidi wowote wa kuthibitisha madai hayo.

Wakati ambao Hunter Biden alipoingia katika mkataba wa gesi asilia katika katika kampuni ya Burisma mwaka 2014, maswali mengi yaliibuka kuwa anaweza kumletea mgogoro kisiasa baba yake.

Ukraine ilikuwa inakabiliana na mgogoro wa kisiasa baada ya kiongozi wake kulazimishwa kuondoka madarakani, wakati huo Biden alikuwa Makamu wa Rais katika utawala wa Barack Obama.

Mwaka 2016, Biden aliisukuma serikali ya Ukraine kumfukuza mwendesha mashitaka Viktor Shokin, ambaye ofisi yake ilikuwa inaichunguza kwa karibu mmiliki wa kampuni ya Burisma.

Katika hotuba yake mwaka jana Biden alijisifia kwa kumfukuza Shokin na kutishia kutotoa mkopo wa mamilioni ya fedha kwa Ukraine.

Trump na washirika wake wanamshutumu Biden kwa kumlinda mwanae.

Kama maofisa wengine wa Serikali ya Ukraine pia walitaka Shokin kuondoka madarakani kwa sababu ya jitihada zake za kukabiliana na rushwa.

Wiki iliyopita mwendesha mashtaka nchini Ukraine ambaye alichukua wadhifa wa Shokin aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC kuwa hakuna ushaidi wa uovu alioufanya Joe au Hunter Biden.

Trump alipohojiwa kuhusu mazungumzo yake ya simu na rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky alijibu kuwa; jibu ni rahisi kuwa ;

“Nilidhani kuwa wameanza kufanya uchunguzi tayari kama kweli walikuwa na nia njema basi wangeanza kumchunguza Biden,”

“Wanapaswa kumchunguza Biden” alisema Trump wakati alipohojiwa na waandishi wa habari katika ikulu ya Marekani.

“Vilevile, China pia inapaswa kuanza kumchunguza Biden kwa sababu kile kilichotokea China ni sawa na kile kilichotokea Ukraine”, Trump aliongeza.

Trump alipendekeza tena bila kutoa ushaidi wowote dhidi ya Biden na kwa kudai uhusiano wa kibiashara kati ya Biden na mataifa hayo mawili, China na Ukraine .

Mkuu wa tume ya uchaguzi aliandika kwenye ukurasa wake wa tweeter kuwa ni kinyume cha sheria kwa mtu yeyote kuhusisha madai ya nchi za kigeni katika uchaguzi wa Marekani.

MAJIBU YA BIDEN

Msemaji wa Biden wa kampeni za mwaka 2020 amemshutumu Trump kwa kutumia vibaya televisheni ya taifa kwa kutoa taarifa za kusadikika.

Naye msemaji wa Hunter Biden ameviambia vyombo vya habari vya Marekani kuwa kiwango cha dola bilioni 1.5 ni hesabu ya uongo, hawajahi kupokea fidia yoyote ya malipo ya kiwango hicho cha fedha katika kiwanda chochote China.

ALICHOFANYA BIDEN

Mwaka 2013,  Biden alipokuwa makamu wa rais alipofanya ziara ya kikazi nchini China na kukutana na rais wa nchi hiyo, Xi Jinping, Hunter Biden na binti yake waliongozana naye.

Biden alikuwa makamu wa rais wa kwanza kuongozana na familia yake katika shughuli za kikazi.

Katika ziara hiyo ya siku mbili , Hunter alikutana mfanyakazi wa benki wa nchini humo, Jonathan Li, ambaye baadae akawa mshirika wake katika biashara.

Li alipata ufadhili binafsi muda mfupi tu baada ya ziara hiyo ingawa msemaji wa Hunter alikiambia chombo cha habari cha NBC News kuwa hawakujadili masuala yoyote ya kibiashara katika ziara ile na ufadhili ulikuja miezi michache baadae.

Hunter amekanusha kuwa na mkutano wowote kuhusu biashara na ofisa wa China.

TRUMP

Uhalifu anaoshutumiwa nao Trump unaweza kumuondoa rais madarakani, na unapitia hatua mbili za mchakato wa kisiasa.

Kama kura za wawakilishi hazitatosha, basi bunge la seneti litalazimika kusimamia kesi hiyo.

Kura ya seneti inahitaji walau wingi wa theluthi mbili ya wingi – na inaweza kushindwa kwa sababu chama cha Trump kina maseneta wengi zaidi.

Ni marais wawili tu katika historia ya Marekani ambao ni Bill Clinton and Andrew Johnson ambao walikabiliana na kesi ya namna hiyo na hakuna kati yao ambaye alishtakiwa au kuondolewa madarakani.

Rais Nixon alijiondoa madarakani kabla ya kung’olewa na bunge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles