25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

‘Masilahi ya wakulima, wafugaji yaangaliwe’

Magembe Makoye
Magembe Makoye

NA JANETH MUSHI, ARUSHA

SERIKALI   imeombwa ifanye mapitio   ya sera na sheria zinazogusa maslahi ya wafugaji na wakulima  kubaini maeneo yanayohitaji maboresho katika utekelezaji.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania, Magembe Makoye alisema hatua hiyo itachangia  ukuaji wa mfumo wa uzalishaji mali, ustawi wa amani miongoni mwa makundi yote.

Alikuwa akizungumza  mwishoni mwa wiki    kwa niaba ya  asasi 36 zisizo za kiserikali zinazotetea haki za wafugaji asili  nchini, baada ya kumalizika  mafunzo ya usalama na tathmini kwa watetezi wa haki za jamii za wafugaji.

Alisema  sera hiyo itasaidia kusimamia haki, rasilimali ardhi na maendeleo ya sekta hiyo kwa vile  sera iliyopo sasa haikidhi maslahi ya mfumo wa ufugaji wa asili, pamoja na elimu kwa wadau kutolewa kwa vyombo vinavyosimamia sheria juu ya haki za binadamu.

“Sekta ya mifugo ni miongoni mwa sekta zilizotekelezwa na Serikali hivyo tunaiomba serikali kwa kushirikiana na wadau kupitia sera hiyo na kuifanyia maboresho   kupunguza baadhi ya changamoto zinazotokea ikiwamo migogoro kati ya wakulima na wafugaji,” alisema Makoye.

Aliiomba Serikali kuharakisha mchakato wa kutenga maeneo ya malisho kwa ajili ya wafugaji    waweze kufanya shughuli zao bila kuingiliwa na wakulima au wawekezaji.

Kuhusu vyanzo vya  migogoro baina ya wakulima na wafugaji, alisema kuwa migogoro hiyo imekuwa ikichangiwa na wafugaji kutokuwa na haki miliki za ardhi na kutokuheshimiwa   mipango halali ya matumizi bora ya ardhi.

Naye Wakili  Benedict Ishabakaki kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), alisema  matukio ya unyanyaswaji wa wafugaji   na watetezi wa wafugaji yakiendelea, wataenda mahakamani kufungua kesi za  katiba.

“Matukio yakizidi kuendelea kutokea tutaenda mahakamani kufungua kesi za  katiba kwa sababu ya matatizo mengi yanayoendelea ya unyang’anyi wa ardhi na manyanyaso kwa watetezi wa haki za wafugaji,” alisema.

Mratibu wa THRDC, Onesmo ole Ngurumwa,   alisema mafunzo hayo yalikutanisha wadau kutoka mashirika na taasisi zinazotetea wafugaji na vyama vya wafugaji kutoka maeneo yote nchini.

 

Alisema lengo ni kuwawekea watetezi  hao mazingira mazuri ya usalama wanapokuwa kazini ikizingatiwa wengi wao wamekuwa hatarini wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles