25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

JET kukutana Julai 23 Dar

John Chikomo
John Chikomo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), kimetangaza kufanyika  mkutano wake mkuu  wa mwaka Julai 23, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa jana   na Mkurugenzi Mtendaji wa JET, John Chikomo, ilieleza kuwa   mkutano huo utakuwa na ajenda sita ambazo zitajadiliwa na wanachama.

“Tunafanya mkutano mkuu wa mwaka   kutimiza masharti na matakwa ya Katiba. Mkutano huu huwashirikisha wanachama wote ambao ni hai wa JET.

“… ndiyo maana nasisistiza hapa wenye haki ya kuhudhuria mkutano huu ni wale   waliolipa ada kwa mujibu wa utaratibu. Ajenda zikazowasilishwa ni kufungua mkutano,

dondoo za mkutano wa mwaka uliopita, yatokanayo na mkutano mkuu uliopita.

“Nyingine ni ripoti utendaji, ripoti mkaguzi wa hesabu na bajeti 2015   na mengineyo,” alisema Chikomo

Mkiurugenzi huyo wa JET alisisitiza kuwa wenye haki kuhudhuria mkutano mkuu huo wa mwaka ni wale tu waliolipa ada zao hadi kufikia Desemba mwaka 2015.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles