27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Baby J apagawisha kwa wimbo wa Bi Kidude

BABY J
BABY J

NA THERESIA GASPER,

MKALI wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), visiwani Zanzibar, Jamilah Abdallah ‘Baby J’ amenogesha uzinduzi wa tamasha la ZIFF  uliofanyika jana katika Hoteli ya Park Hyatt, visiwani Zanzibar kwa kuimba wimbo wa ‘Mhogo wa Jangombe’, ulioimbwa na marehemu Bi Kidude.

Taratibu wimbo huo uliokuwa ukinogeshwa kwa ala za ‘live’ na sauti nzuri ya Baby J ulianza kumuinua Waziri wa Afya Zanzibar, Thabit Kombo, kisha Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Profesa Martin Mhando na baadhi ya wadhamini wa tamasha hilo waliinuka na kujumuika kucheza kwa madaha wimbo huo huku wakimtunza fedha mwimbaji huyo.

Wengi wakiushangilia wimbo huo, Baby J alimuomba Waziri wa Afya ajumuike naye na kuimba pamoja ambapo waziri huyo alijongea kwenye kipaza sauti na kuimba huku umati wa watu ukilipuka kwa sauti za shangwe.

Naye Baby J alifurahishwa na kitendo cha viongozi, wafanyabiashara na wadhamini wa tamasha hilo walivyojumuika naye katika wimbo huo huku akishukuru uongozi wa Ziff kwa kumchagua yeye kati ya wasanii wengi wenye uwezo wa kuimba wimbo wa Bi Kidude.

“Nimefurahishwa sana na namna viongozi walivyopokea vema na kujumuika kucheza nami katika wimbo wa ‘mhogo wa Jang’ombe’ wa Bi Kidude wakati wa uzinduzi huo. Imenihamasisha na imeniongezea nguvu kufanya makubwa zaidi,’’ alisema Baby J.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles