24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MASHIRIKA YAZIDI KUONGEZA NGUVU KUTOKOMEZA UJANGILI

Ndege ndogo iliyotelewa na Shirika lisililo la kiserikali la PAMS kwa ajili ya kufanya doria angani, katika pori la wanyama Korido la Nyasa na Selous.

 

 

Na AMON MTEGA, TUNDURU

ILI kufanikiwa kukabiliana na majangili kwenye hifadhi za Taifa nchini, jamii inayoishi karibu na maeneo husika pamoja na wadau mbalimbali wanapaswa kuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo hivyo.

Vitendo vya kijangili vimekuwa virudisha nyuma jitihada za serikali za kuinua uchumi kwa kupitia sekta ya Maliasili na Utalii.

Wanyama ambao wamekuwa wakiwindwa kwa kasi zaidi ni tembo, faru na wale wadogo wagodo, ambao hufanywa kitoweo, pia huuzwa kwa watui wanaishi karibu na hifadhi husika.

Kutokana na hali hiyo, hivi majuzi Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Juma Homela amelipongeza shirika lisilo la kiserikali la PAMS Foundation linalofanya kazi kwa  kushirikiana na askari wa wanyamapori kulinda wanyama wanaouawa kwa kasi kwenye korido la Nyasa katika pori la Selous.

Pongezi hizo alizitoa wakati akizungumza na viongozi wa idara hiyo kutoka makao makuu ambao waliwasili wilayani hapo katika Kijiji cha Wenje, kufuatia kuuawa kwa tembo wawili huku mmoja akiwa na mimba hivyo kufanya jumla ya tembo watatu.

Homela anasema kuwa kama jamii itatambua umuhimu wa kulinda wanyama hao kama linavyofanya shirika la PAMS, vitendo hivyo vitapungua au kutokomea kabisa kwa kuwa wanaofanya uhalifu huo ni wakazi wa maeneo jirani.

Anasema shirika hilo limeonyesha njia sahihi ya kukabiliana na vitendo hivyo, kilichobaki ni wanajamii wa maeneo husika kuungana na jitihada hizo ili kuwanusuru wanyama ambao wamekuwa wakitoweka kwa kuuawa na majangili.

Anasema kitendo cha kuwapo kwa ndege mbili ndogo zilizotolewa na shirika hilo kumesaidia kupunguza vitendo vya kijangili kwenye pori hilo  kutokana na kuongeza nguvu kwa askari wa wanyamapori kwa kuwarahisishia kazi ya kutambua majangili walipojificha.

Anafafanua kuwa kutokana na kuwapo kwa vitendea kazi hivyo, baadhi ya vijiji vimepunguza malalamiko ya kuingiliwa na wanyama hao kwa kuwa wamekuwa wakifukuzwa mapema kabla ya kwenda kuvamia makazi ya binadamu tofauti na kipindi cha nyuma.

“Kipindi cha nyuma baadhi ya vijiji ambavyo vipo karibu na korido hiyo, wananchi wake walikuwa wakilalamikia vitendo vya wanyama hasa tembo kuingia kwenye mashamba ya wanavijiji,” anasema.

Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa kuzuia ujangili Taifa, Robart Mande anasema Serikali ya awamu ya tano imejipanga kikamilifu kukabiliana na vitendo vya kijangili hivyo kila mwananchi awe mstari wa mbele kukemea vitendo hivyo viovu.

Anasema thamani ya tembo ni kubwa mno hivyo wanapaswa kutunzwa.

Anataja thamani ya tembo mmoja kuwa ni Dola za Marekani 15,000. Fedha ambazo ni mali ya Watanzania wote.

Naye Mratibu wa shirika la PAMS Foundation, Maximillan Jenes anasema watazidi kuungana na serikali kuongeza nguvu ya kuhakikisha vitendo vya kijangili vinakomeshwa.

Jenes anasema kwa sasa ndege hizo mbili zinafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanyama wanalindwa.

Katika tukio la kuuawa kwa tembo hao lililotokea Aprili 18 mwaka huu, watu wanane wanaodhaniwa kuhusika na mauaji hayo wanashikiliwa na polisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles