23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Mashine ya kuangalia mapigo ya moyo, upumuaji yaibwa hospitali

Na Derick Milton, Simiyu

Katika hali asiyokuwa ya kawaida mashine inayotumika kuangalia maendeleo ya mgonjwa wakati wa upasuaji ikiwemo mapigo ya moyo, wingi wa hewa ya Oksijeni kwenye damu pamoja na upumuaji imeibwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.

Kifaa hicho kinadaiwa kuibwa usiku wa kuamkia Jumapili Septemba 20, 2021, kikiwa katika chumba cha upasuaji mkubwa namba mbili katika hospitali hiyo.

Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Mike Mabimbi amesema kuwa upotevu wa kifaa hicho uligundulika baada ya mmoja wa madaktari siku ya jumatatu asubihi kuhitaji kutumia mashine hiyo.

Amesema kuwa Daktari huyo (hakumtaja jina) mara baada ya kufika katika chumba hicho kwa ajili ya kutaka kumpima mgonjwa, ndipo aligundua kutokuwepo kwa mashine hiyo.

“Mashine yenyewe ndiyo ambayo imechukuliwa, huku stendi yake ikiwa imeachwa, pamoja na vifaa vingine, mazingira yanaonyesha kuwa mashine hii iliibiwa usiku wa kuamkia siku ya jumapili wiki iliyopita,” amesema Mabimbi.

Aidha, Dk. Mabimbi amesema kuwa siku ya Alhamisi, ijumaa na jumamosi wakati wanafanya ukaguzi kwenye vyumba vyote vitatu vya upasuaji, mashine hiyo ilikuwepo.

Amesema kuwa watumishi sita ambao wamekuwa wakifanya kazi kwenye chumba hicho, wakiwemo madaktari watatu na wauguzi watatu wamehojiwa na uongozi wa hospitali hiyo kujua mazingira ya upoteaji wa kifaa hicho.

“Kati ya watumishi wote sita, mmoja amegoma kuhojiwa, wengine wote wamekana kuhusika na wizi huo na wanadai kuwa kifaa hicho walikiacha mara baada ya kazi,” amesema Mabimbi.

Aidha amesema kuwa kutokana na hali hiyo wametoa taarifa jeshi la polisi na kufungua kesi BRD/RB/2342/2021 ikiwa pamoja na kutoa taarifa Wizara ya Afya kwa ajili ya hatua nyingine zaidi.

Dk. Mabimbi amewataka watu ambao wamehusika na wiza wa kifaa hicho, kukirejesha mara moja kwani serikali ilikileta kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.

Ikumbukwe kuwa Agosti 5, 2019 majira ya mchana Dk. Mike Mabimbi akiwa Mganga Mfawidhi hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi (Somanda) iliibwa mashine inayotumika kupima magonjwa ya ndani na kutambua taarifa katika mwili wa binadamu (ultrasound).

Soma pia: (https://mtanzania.co.tz/mashine-ya-ultrasound-yaibwa-mazingira-kutatanisha-hospitali/)

Hata hivyo Dk. Mabimbi alihamishwa na kupelekwa Wizara ya Afya kabla ya kurejeshwa katika mkoa wa Simiyu na kuwa Mgamga Mfawidhi wa hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa ikiwa ni miezi miwili tu na wizi huo ukatokea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles