27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi wajipanga kutoa Tuzo kwa shule zenye ufaulu mzuri

Na Malima Lubasha, Serengeti

Jumuiya wa Wazazi Mkoa wa Mara imeazimia kutoa hati ya pongezi kwa shule zote za sekondari zilizofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita kaa njia ya kuhamasisha maendeleo ya elimu.

Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa, Julius Kambarage alipozungumuza na viongozi junuiya hiyo ngazi ya kata wilayani Serengeti huku akihimiza wanachama kujisajili kupata kadi za kielektroniki.

Hatua hiyo inakuja kufuatia taarifa iliyotolewa kuhusu ufaulu wa shule ya Shule ya Sekondari Natta iliyopo wilayani humo ambayo imefanya vizuri na kuweza kushika nafasi ya 13 kitaifa kwa matokeo ya mtihani wa kidato cha sita na kuongoza kimkoa.

Alisema Jumuiya ya wazazi inaamini tuzo na vyeti vya pongezi vitasaidia kuwatia moyo walimu kuongeza bidii katika kazi yao ili waendelee kufanya vizuri katika ufundishaji hivo kuinua kiwango cha taaluma wilayani humo.

“Nawataka wazazi na walezi wote Mkoani Mara kuguswa na matokeo ya Shule ya sekondari ya Natta na wao wahakikishe wanafuatilia maendeleo na mahudhurio ya watoto shuleni” alisema Kambarage.

Hata hivyo Kambarage aliwahimiza wananachi kujitolea kujenga shule za sekondari karibu na maeneo gao ili kuondoa adha ya watoto kutembea umbali mrefu na kuwakinga watoto wa kike dhidi ya vishawishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles