25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Maafisa elimu na Takukuru watakiwa kuelimisha jamii kuhusu madhara ya rushwa

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi amewataka maafisa elimu Mikoa na Wilaya pamoja na Maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuhakikisha wanatenga muda wa kuelimisha vijana na jamii kwa ujumla kuhusu madhara ya rushwa.

Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 23, 2021 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa Mkakati wa makubaliano baina ya Takukuru na Chama cha Skauti Tanzania wenye lengo la kusisitiza ushirikishwaji wa wadau katika mapambano dhidi ya rushwa kuanzia ngazi ya chini.

Naibu Waziri huyo amesema muongozo wa mkakati wa makubaliano kati ya Chama cha Skauti Tanzania na Serikali utasaidia kujenga uchumi imara na kuchochea maendeleo ya huduma za kijamii.

Ndejembi amewataka maafisa elimu Mikoa na Wilaya na Maafisa wa (TAKUKURU), kuhakikisha wanatenga muda wa kuelimisha vijana na jamii kwa ujumla  kuhusu madhara ya rushwa.

Amesema Muongozo huo pia unajenga kuelimisha jamii kuacha vitendo vya rushwa huku akitoa maelekezo. 

Ndejembi amesema kutokana na kwamba vijana wengi wa Skauti wapo masomoni itakuwa rahisi kwao kufanya uelimishaji kupitia makundi mbalimbali huku akitoa agizo kwa wanufaika mafunzo hayo kupeleka kwa jamii elimu wanayoipata Kuhusu suala la rushwa.

Amesema Serikali  itaendelea kuunga mkono juhudi hizo na kuleta mafanikio ambayo yatafikisha ujumbe kimataifa kwamba Skauti ni kundi muhimu linaloshiriki kurudisha haki kwa kuzingatia uzalendo na uwajibikaji.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU, Neema Mwakalyelye amesema mwaka 2019 walisaini mkataba wa makubaliano na chama cha Skauti Tanzania katika mapambano dhini ya rushwa na malengo ya mashirikiano hayo ni kuelimisha jamii madhara ya rushwa katika jamii .

Amesema kupitia mkakati huo,wanatarajia kuongeza upana wa makundi ya mapambano dhidi ya rushwa nchini ambapo kuna takriban vijana 105 wamenufaika na mafunzo hayo.

Naye, Skauti Mkuu Mwantumu Mahiza amewataka   viongozi na Wakuu wa idara  kuwapa ruhusa watumishi wa Umma kushiriki masuala ya Skauti pindi wanapohitajika na kuwapatia ruzuku kwa ajili ya kujikimu Kwa kuwa kada hiyo haina fungu la ruzuku kwa wananchama wake.

“Ziko baadhi ya Taasisi ambazo hadi sasa hazielewi wala kutilia  maanani masuala ya skauti, kupitia hili naomba Serikali itoe mwongozo ili vijana wetu wa Skauti wasidhalilike,Skauti sio uhuni, vijana hawa wana thamani, wasomi na waadilifu lazima tuwaheshimu,” amesema.

Skauti huyo ameiomba serikali kuwaona vijana hao wa Skauti pindi linapokuja suala la uteuzi wa viongozi na kuihakikishia Serikali kuwa vijana hao ni waadilifu na wawajibikaji wasiopenda rushwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles