23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Mashinji aja na mikakati kuinua elimu Serengeti

Na Malima Lubasha, Serengeti

Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, Dk.Vicent Mashinji ameweka wazi mikakati mipya kwa ajili ya kuinua kiwango cha ufaulu wilayani humo na kuweza kufikia adhima ya maendeleo endelevu kwa wananchi.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani ikiwa ni kikao chake cha kwanza cha Halmashauri hiyo, Dk. Mashinji alisema mikakati iliyowekwa iwapo itatekelezwa vizuri, kusimamiwa kwa weledi na kila kiongozi itasaidia kufanikisha mapinduzi ya kiuchumi.

Alitaja mikakati hiyo ni kuwekea mkazo na usimamizi wa suala la ulinzi na usalama, mapato ya Halmashauri, Usafi, Mikopo asilimia 10, asilimia 40 ya mapato ya Halmashauri kwenda kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ile ya elimu, uwekezaji na kukomesha suala la utoro mashuleni.

Alisema wilaya haiwezi kupiga hatua ya maendeleo kama viongozi hawatasimama kidete mikakati hiyo ambapo aliwataka madiwani ambao ni wawakikilishi wa wananchi kusimama mstari wa mbele kuhakikisha hayo yanatekelezwa kikamilifu na kwa ufanisi.

Alisema hadi sasa hali ya ulinzi na usalama wilayani humo ipo salama na uharifu umeweza kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa ambapo aliwataka viongozi kuendeleza hali hiyo huku akiagiza wananchi kupatiwa elimu juu ya umuhimu wa hifadhi ya taifa ya Serengeti ili kupunguza uharifu hifadhini.

AidhaMkuu huyo wa Wilaya Dk. Mashinji alisisitiza na kuwataka madiwani kuhakikisha wanahamasisha na kuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa mapato sambamba na kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato ili kusaidia ukamilishaji wa miradi ya maendeleo.

Aidha aliwata Madiwani hao kuweka mikakati ya kudhibiti utoro shuleni na kusimamia mahudhurio ya watoto shuleni hasa huku akiagiza walimh wakuu, watendaji wa vijiji kama wadau wengine qa wa elimu kufanya msako wa watoro na kuwachukulia hatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles