26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

MASHABIKI MADRID WATAKA MESSI AFUNGIWE

MADRID, HISPANIA

MASHABIKI wa klabu ya Real Madrid, wamekuja juu kwenye mitandao ya kijamii huku wakitaka mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi, afungiwe michezo kadhaa kutokana na kumshika bega mwamuzi.

Staa huyo wa timu ya Taifa ya Argentina, Jumanne wiki hii aliisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Juventus kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa huku akifunga mabao mawili peke yake.

Kwenye mchezo huo, Messi alioneshwa kadi ya njano katika dakika ya 54, baada ya kumshawishi mwamuzi wa mchezo huo atoe kadi ya njano kutokana na kuchezewa vibaya, hata hivyo mbali na kumshawishi mwamuzi atoe kadi, alionekana akimshika bega mwamuzi kumlazimisha atoe kadi.

Hata hivyo, mwamuzi aliamua kumwonesha Messi kadi ya njano badala ya mchezaji ambaye alimchezea vibaya mshambuliaji huyo.

Katika sheria za soka nchini Hispania, zinadai kuwa mchezaji akimfuata mwamuzi na kumsukuma au kumshika kwa lengo la kumshawishi jambo lolote uwanjani, anastahili kufungiwa michezo minne hadi 12.

Mwezi uliopita mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, alifungiwa michezo mitano kutokana na kumsukuma mwamuzi kwenye mchezo wa Kombe la Supercopa, huku Madrid ikishinda mabao 3-1.

Mchezaji huyo awali alioneshwa kadi ya njano kutokana na kushangilia huku akiwa amevua jezi na baadaye alioneshwa kadi ya pili ya njano na nyekundu baada ya kujiangusha kwenye eneo la 18 akimshawishi mwamuzi Ricardo de Burgos Bengoetxea, ampe penalti. Ronaldo baada ya kuoneshwa kadi nyekundu, aliamua kumsukuma mwamuzi huyo jambo ambalo lilimpelekea kufungiwa michezo mitano kutokana na sheria ya soka nchini humo.

Mbali na mchezaji huyo kufungiwa michezo mitano, lakini alitakiwa kulipa faini ya Euro 800 ni sawa na Sh 2,116,750 za Kitanzania.

Kutokana na hali hiyo, mashabiki wa Real Madrid, wamedai kitendo alichokifanya mshambuliaji wa Barcelona, Messi ni sawa na Ronaldo, hivyo anatakiwa kuchukuliwa hatua.

Ronaldo juzi alirudi dimbani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuisaidia timu yake kushinda mabao 3-0 dhidi ya Apoel Nicosia, huku mchezaji huyo akipachika mabao mawili peke yake na bao lingine likipigwa na Sergio Ramos.

Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa juzi ni pamoja na Liverpool wakitoka sare ya 2-2 dhidi ya Sevilla, Porto wakipigwa 3-1 dhidi ya Besiktas, Tottenham ikishinda mabao 3-1 dhidi ya Dortmund, wakati huo Maribor ikitoka sare 1-1 dhidi ya Spartak Moskva na RB Leipzig wakitoka 1-1 dhidi ya Monaco.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles