30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MO AMPONZA MAVUGO SIMBA

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

NI wazi mshambuliaji Laudit Mavugo sasa ataanzia benchi katika michezo ijayo ya Simba ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ukiwamo wa Jumapili dhidi ya Mwadui FC, ili kutoa nafasi kwa kiungo Mohamed Ibrahim ‘Mo’ kuanza.

Kocha wa Simba, Joseph Omog, tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu amekuwa akimtumia Mo kama mchezaji wa akiba, huku akimpa nafasi ya kuanza Mavugo.

Mavugo, licha ya kupata nafasi hiyo, ameshindwa kuthibitisha ubora wake, baada ya kushindwa kupachika bao hata moja katika mechi mbili za Ligi Kuu ambazo Simba imecheza hadi sasa, zikiwamo dhidi ya Ruvu Shooting ilipoibuka na ushindi wa mabao 7-0 na Azam FC uliokwisha kwa suluhu.

Wakati Mavugo akipata bahati hiyo na kushindwa kuitumia, Mo licha ya kutokea benchi, amekuwa akionyesha kiwango maridadi, hatua iliyowafanya mashabiki wa Simba kuhoji sababu za kutopangwa katika kikosi kinachoanza.

Kilio cha mashabiki wa Simba kinaonekana kumfikia kocha wao, Omog, ambaye katika mazoezi ya timu hiyo jana kwenye Uwanja wa Uhuru, alionekana kumpanga Mo katika kikosi cha wachezaji 11 ambao wamekuwa wakianza katika michezo iliyopita.

Kikosi hicho kiliundwa na kipa Emmanuel Mseja, John Bocco, Salim Mbonde, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Nicholas Gyan, James Kotei, Mohamed Ibrahim ‘Mo’, Juuko Murshid, Ally Shomary, Emmanuel Okwi, Mzamiru Yassin na Mo.

Kikosi kilichoonekana cha akiba katika mazoezi hayo kilikuwa na Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Mavugo, Said Ndemla, Yusuph Mlipili, Jamal Mnyate,  Jamal Mwambeleko, Method Mwanjale, Shiza Kichuya na Aishi Manula.

Katika mazoezi hayo, vikosi hivyo viwili vilicheza bonge la mechi, ambapo kikosi chao kilichoonekana cha kwanza kililazwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles