20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

SERENA WILLIAMS AMWANIKA MWANAWE

NEW YORK, MAREKANI

ALIYEKUWA bingwa namba moja wa mchezo wa tenisi duniani kwa upande wa wanawake, Serena Williams, hatimaye amemweka wazi mtoto wake kwa mara ya kwanza tangu ajifungue Septemba 1, mwaka huu.

Bingwa huyo mwenye umri wa miaka 35, ambaye kwa sasa anashika nafasi ya 22 kwa ubora, ameposti picha na video za mtoto wake huyo wa kike kisha kukielezea kipindi cha wiki mbili tangu ajifungue.

“Huyu ndiye mtoto ambaye nimempata, anaitwa Alexis Olympia Ohanian, furaha kubwa kuwa mama wa familia, akiwa kama mtoto wa kwanza amenifanya niyajue mambo ambayo nilikuwa siyajui, tumekaa siku sita hospitalini kutokana na mambo mbalimbali ambayo yalikuwa yanatusumbua,” alisema Serena.

Hata hivyo, Serena hakutaka kuyaweka wazi matatizo ambayo alikutana nayo na mtoto wake mara baada ya kuzaliwa huku akiwa na kilo sita.

“Safari ya ujauzito ni ndefu, kulikuwa na changamoto mbalimbali ambazo kwangu niliziona mpya kwa kuwa yalikuwa maisha ambayo sijawahi kuyapitia, lakini kwa sasa ninashukuru kwa kufanikiwa kuzipita salama.

“Wakati nina ujauzito wa wiki mbili nilifanikiwa kucheza kwenye michuano ya Australian Open, hapo nikagundua kwamba atakuwa mtoto wa kike kwa kuwa nilicheza kwenye mazingira magumu ambayo ingekuwa mtoto wa kiume angeanza kunisumbua, lakini baada ya kuona kuwa niko sawa nikajua kuwa ni mtoto wa kike.

“Najua mtoto wa kiume hapendi usumbufu tofauti na wa kike, lakini mume wangu hakuamini nilipomwambia kuwa mtoto wetu atakuwa wa kike hadi pale nilipojifungua,” aliongeza.

Hata hivyo, Serena ameweka wazi kuwa atarudi kwenye tenisi baada ya miezi mitatu tangu ajifungue kwa kuwa mchezo huo ni sehemu ya maisha yake.

“Najua baada ya miezi mitatu nitakuwa katika hali nzuri kiafya na mwanangu nitamuacha akiwa sawa,” alisema Serena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles