31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

PAUL POGBA NJE WIKI SITA

MANCHESTER, ENGLAND

KLABU ya Manchester United, imethibitisha kuwa kiungo wao, Paul Pogba, atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Basel wiki hii.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, alipatwa na tatizo la nyama za paja katika dakika ya 19 ya mchezo huo kabla ya klabu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Manchester United wamedai kwamba, mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kabla ya wiki mbili zinazofuata kuanza mazoezi mepesi na anaweza kurudi kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England dhidi ya Liverpool, Oktoba 14.

Kipindi hiki ambacho mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja ataikosa baadhi ya michezo kama vile Everton mwishoni mwa wiki hii, Southampton, Crystal Palace pamoja na Kombe la Ligi mzunguko wa tatu dhidi ya Burton na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya CSKA Moscow, Septemba 27.

Hata hivyo, mchezaji huyo atakosa kuitumikia timu yake ya Taifa ya Ufaransa kwenye michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi dhidi ya Bulgaria na Belarus mapema Oktoba.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, mchezaji huyo aliposti picha akiwa na mama yake pamoja na kaka zake mapacha Florentin na Mathias, huku mchezaji huyo akiwa amesimama na magongo.

“Nilikuwa sijui nitakuwa nje kwa muda gani, lakini kwa sasa ninajua kwamba kuna uwezekano wa kukaa kwa muda wa mwezi mmoja, kutokana na uzoefu wangu ni kwamba ukiwa na tatizo la nyama za paja unaweza kuwa nje kwa wiki kadhaa.

“Niwatoe wasiwasi mashabiki wa Manchester United kwamba ninaamini nitakuwa katika hali yangu ya kawaida baada ya wiki chache, nashukuru kwa sapoti yenu,” aliandika Pogba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles