27.1 C
Dar es Salaam
Sunday, February 5, 2023

Contact us: [email protected]

Mashabiki Chelsea waitaka jezi ya Hazard

eden-hazard_afp_3085313bLONDON, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa timu ya Chelsea, Eden Hazard, juzi alikuwa katika wakati mgumu baada ya kubadilishana jezi na kiungo mshambuliaji wa PSG, Di Maria, hivyo mashabiki walitaka jezi hiyo kurudishwa.

Mshambuliaji huyo ambaye inasemekana kwamba anatarajia kujiunga na klabu hiyo ya PSG msimu ujao, katika mchezo wa juzi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya alibadilishana jezi na Di Maria wakati wa mapumziko huku klabu hizo zikiwa zimefungana 1-1.

Hali hiyo ilileta gumzo kwa mashabiki kutokana na kitendo hicho cha mchezaji wao kubadilishana jezi wakati dakika 90 hazijamalizika.

Kitendo hicho kimeleta maana mbaya kwa mashabiki ambapo wengi wao wakidhani kwamba mchezaji huyu yuko mbioni kujiunga na wapinzani hao.

Hata hivyo, katika mchezo huo Hazard hakumaliza dakika 90 ambapo alitolewa huku zikiwa zimebaki dakika 13 mchezo huo kumalizika na mashabiki wakaanza kumzomea mchezaji huyo.

Tukio kama hili liliwahi kumtokea mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Liverpool, Mariao Balotelli ambapo alibadilishana na beki wa Real Madrid, Pepe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa mwaka 2014.

Mchezaji mwingine ambaye aliwahi kufanya tukio kama hilo ni beki wa zamani wa Arsenal, Andre Santos alipobadilishana jezi na Van Persie wakati wa mchezo wa Manchester United dhidi ya Arsenal, huku Arsenal ikishinda mabao 2-1 mwaka 2012.

Katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, PSG imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali baada ya kuichapa Chelsea mabao 2-1 na kuwa jumla ya mabao 4-2 pamoja na mchezo wa awali, wakati huo Benfica wakishinda mabao 2-1 na kuwa jumla ya mabao 3-1. Hivyo PSG, Benfica zinaungana na Real Madrid na Wolfsburg hatua ya robo fainali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles