Teyana Taylor avishwa pete ya uchumba

0
797

Teyana-Taylor-Iman-Shumpert-bet-awards-2015-billboard-650LAS ANGELES, MAREKANI

MSANII wa muziki na filamu nchini Marekani, Teyana Taylor, amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, Iman Shumpert, ambaye ni mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Cleveland Cavaliers.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 25, amesema umri wake umefikia hatua ya kuolewa na tayari amempata mwanamume sahihi katika maisha yake.

“Nilikuwa nikisubiri muda kufanya maamuzi haya, nadhani huu ni umri wangu sahihi wa kuolewa, nashukuru nimempata mwanamume sahihi, tumekubaliana kuoana.

“Nimemchunguza na yeye amefanya hivyo na ndiyo maana tumefikia hatua hii, suala la ndoa likiwa tayari tutaliweka hadharani kama ilivyo kwenye jambo hili la kuvishwa pete.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here