Tyga: Tupac alikuwa zaidi ya baba yangu

0
1258

tygaNEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Michael Stevenson ‘Tyga’, amesema kwamba alikuwa akimkubali mwasisi wa muziki huo, Tupac Shakur, kuliko baba yake mzazi.

Msanii huyo amesema Tupac amefanya maisha yake yawe hivyo, huku akidai anaendelea kuiga maisha yake.

“Nimekuwa katika maisha bila ya baba yangu, hivyo nilitokea kumpenda Tupac zaidi ya baba na niliamua kubadilisha aina ya maisha yangu kuwa kama yeye,” alieleza Tyga.

Msanii huyo, kupitia akaunti yake ya Instagram, aliiweka picha yake sambamba na ya Tupac, huku akiandika ‘Wewe ni baba kwangu’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here