29.7 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Sunderland yamsajili Eboue

Emmanuel-EbouéSUNDERLAND, ENGLAND

KLABU ya Sunderland imefanikiwa kumsajili nyota wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Eboue kwa mkataba wa muda mfupi.

Klabu hiyo imethibitisha kumsajili beki huyo raia wa Ivory Coast ambaye alikuwa akifanya nao mazoezi kwa kipindi cha wiki kadhaa mara baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Galatasaray ambaye aliitumikia kwa miaka minne huku akichukua mataji ya ligi mara tatu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, mkataba wake katika klabu ya Sunderland utamalizika hadi mwishoni mwa msimu huu.

“Nimekuwa na furaha kubwa kuwa mchezaji wa Sunderland, wakati naanza kufanya mazoezi nilijiona kama nilikuwepo hapa siku za nyuma, ndoto zangu zilikuwa hivi wakati nipo nchini Uturuki kwa kuwa niliwahi kucheza Ligi ya England hapo awali, ninawashukuru viongozi wa klabu hii kwa kunichukulia kama mtoto wao.

“Tuna kazi ngumu ya kuhakikisha klabu hii inapanda juu katika msimamo wa ligi kwa kuwa sasa tupo chini sana na ni hatari katika Ligi Kuu,” alisema Eboue.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles