Masanja asakwa na polisi akiwa ‘honeymoon’

13932841_327351570938329_5565219885105093686_n

NA ASIFIWE GEORGE,

WAKATI dhamana ya waigizaji wa kundi la Orijino Komedi ikiwa wazi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeanza kumsaka bwana harusi, Emmanuel Mgaya, kwa mahojiano kama walivyofanya kwa wenzake.

Hayo yameelezwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Hezron Gyimbi, jana baada ya kuwahoji waigizaji hao waliokuwa wakishikiliwa na jeshi hilo tangu juzi kwa kosa la kuvaa mavazi yanayofanana na ya jeshi hilo.

Waliokamatwa na kuwekwa ndani hadi jana ni kiongozi wa kundi hilo, Sekioni David, Alex  John ‘MacRegan’, Isaya Gideon ‘Mama Bele’ na Lucas Lazaro ‘Joti’.

Kamanda Gyimbi alisema wasanii hao walikamatwa wakiwa na kofia, filimbi, shati, suruali, mkanda pamoja na cheo na licha ya dhamana yao kuwa wazi baada ya kukamilisha masharti wanaendelea kumtafuta bwana harusi, Masanja Mkandamizaji, aliyekuwepo katika mapumziko ya harusi yake.

“Upelelezi unaendelea lakini bado tunamsaka Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ ili naye tumuhoji kama tulivyowahoji wasanii wenzake, lakini kwa kuwa upelelezi wa jambo hili unaendelea hivyo hatutatoa maelezo ya walipopata sare hizi za jeshi na mambo mengine hadi tutakapokamilisha upelelezi wetu,’’ alieleza Kamanda Gyimbi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here