Jamii yatakiwa kufichua wezi wa kazi za wasanii

Scholastica Kevela
Scholastica Kevela
Scholastica Kevela

Na WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM

JAMII imeombwa kuwafichua wanaotumia vibaya kazi za wasanii na kujinufaisha nazo huku wasanii hao wakibaki masikini.

Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa albamu ya msanii wa nyimbo za injili, Lilian Germin, Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Yono, Scholastica Kevela, alisema kazi nyingi za wasanii hasa wa muziki wa injili zimekuwa zikiuzwa isivyo halali na kuikosesha mapato Serikali na wasanii husika.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kisima cha Makimbilio lililoko Kimara Kilungule, Benedict Lyimo, alisema injili inayotangazwa kwa njia ya uimbaji huwafikia na kuwakomboa watu wengi.

Hata hivyo, Kevela alichangia Sh 700,000 kwa ajili ya uzinduzi wa albamu hiyo yenye jumla ya nyimbo saba ambazo ni ‘Ahsante bwana yesu’, ‘Haleluya’, ‘Roho mtakatifu’, ‘Tawala bwana’, ‘Wewe ni bwana uniwezeshaye’ na ‘Wewe ni mwema’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here