25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 19, 2022

MAREKANI KUANZA KUTUMIA ‘NYUKI’ KUFANYA MASHAMBULIZI

 

 

Na JUSTIN DAMIAN,

MAREKANI inaendelea kuimarisha teknolojia zake za kivita na sasa wanaweza kutumia ndege ndogo zinazojiendesha zenyewe ambazo huruka kwa wingi kama kundi la nyuki.

Ndege hizo zinazoitwa Perdix, zinaouwezo wa kudhoofisha silaha za adui, kufanya ujasusi pamoja na mashambulizi hatari zaidi kwa njia ya anga.

Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo (Pentagon) tayari imeshafanya majaribio ya ndege-nyuki hizo ambazo zinaelezewa kuwa zinatumia gharama ndogo kuzitengeneza huku zikiwa pamoja na mambo mengine uwezo mkubwa wa kuharibu au kuchanganya mfumo wa ulinzi na mawasiliano wa maadui

Pentagon imefanya majaribio kwa ndege-nyuki hizo 103 ambazo ziliruka kwa pamoja na kuonyesha ufanisi wa hali ya juu na kupewa hadhi ya ‘silaha hatari.’ 

Ndege nyuki hizo za kwanza kutengenezwa, zinaweza kutumika kama kamera za kijasusi kuonyesha namna magaidi au maadui wanaojaribu kutoroka.

Uwezo wa kutengeneza akili zisizo za kibinadamu (artificial intelligence) zimewawezesha wanasayansi kutengengeneza roboti wanaoweza kufanya kazi kwa pamoja. Kwa sababu Perdix zinaweza kuwasiliana zenyewe kwa zenyewe, hazihitaji kuongozwa.

Perdix (pichani) zenye urefu wa sentimita 16, zimewekewa mfumo wa mawasiliano wa radio pamoja na kamera. Zina uwezo wa kutoa na kupokea mawasiliano kutoka nje

Wakati zikielezewa kama chombo cha kufanya ujasusi, gazeti la Washington Post la Marekani linasema ndege-nyuki hizo zinaweza kutumika kufanya mashambulizi ya mbali ya mabomu.

Wataalamu wa mikakati ya kijeshi wanasema, wana matumaini makubwa kuwa Perdix zitakuwa rahisi kuzalishwa kwa wingi na kuwa na uwezo mkubwa wa kudhoofisha mfumo wa ulinzi wa adui kutokana na wingi wake kama ilivyo kundi la nyuki.

Majaribio ya kundi kubwa la ndege-nyuki duniani lilifanyika Desemba katika Jimbo la California, ambalo lilihusisha Perdix 103,” inasomeka sehemu ya taarifa iliyotolewa na Pentagon.

“Perdix inao uwezo wa kuchanganya mfumo wa ulinzi wa anga wa adui. Zikiwa na mfumo wa mawasiliano wa kielectroniki, zinaweza kufanya mfumo wa rada wa adui ushindwe kufanya kazi.

“Perdix hazifanyiwi utaratibu wa mawasiliano kwa moja moja, badala yake huwekewa uwezo wa kuwasiliana kwa pamoja kupitia ‘ubongo’ mmoja. Kwa hiyo uamuzi hufanyika sehemu moja na utekelezaji wake huwa ni wa pamoja kama ilivyo kwa kundi la nyuki,” anasema Dk. William Roper, Mkurugenzi wa Mikakati ya Kivita wa Pentagon.

Katibu anayehusika katika iadara ya ulinzi Ash Carter, ambaye aliwahi kuwa Profesa katika Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani, alitengeneza mfumo wa kujilinda ambao ulifanana kwa mbali na huuwa Perdix kwa mara ya kwanza wakati akiwa naibu wa masuala ya ulinzi mwaka 2012.

Idara hiyo imepewa jukumu la kufanya utafiti na kuingiza teknolojia mpya na za kisasa katika ulinzi kupitia silaha zenye kutumia teknalojia ya hali ya juu zitakazongeza ufanisi.

Pamoja na uwepo wa teknolojia ambazo zimekuwa zikitumika kibiashara, ugunduzi huu wa Perdix umekuwa wa aina yake na unatarajia kuleta mapinduzi ya utengenezaji silaha zenye ufanisi kwa gharama nafuu.

Kwa mara ya kwanza Perdix zilitengenezwa na mwanafunzi wa uhandisi katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts mwaka 2013 na ziliendelea kuboreshwa mpaka hatua ambayo imefikiwa leo.

Majaribio ya kwanza yalifanyika kwa kutumia ndege tatu za kivita aina ya F-18 ambazo ziliruka na kuachia ndege nyuki hizo katika anga la jangwa la California nchini Marekani.

Perdix hutoka kwenye F-18 kama parachute na baadaye parachute hilo hupasuka kisha kutoka na kusambaa kwa kasi.

Perdix zinaweza kufanya mashambulizi ambayo ni hatari au magumu kufanywa na binadamu na zinaelezewa kama mapinduzi mapya katika medani ya mapigano ya kivita.

Tofauti na wanajeshi ambao wanahitaji kupewa amri ya kufanya jambo fulani, wataalamu wanaoziongoza hutoa maelekezo ya jumla na mambo mengine huweza kujiamulia zenyewe kutokana na mazingira. Kwa mfano; wakati wa majaribio zilipewa amri ya kufanya patro eneo lenye urefu wa maili tatu lakini hazikuambiwa zifanye kwa njia gani.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
175,234FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles