26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 18, 2022

KITABU APP: NJIA PEKEE KUHAMASHA USOMAJI VITABU

Mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa akielezea namna ya kupakua Kitabu App kwa watumiaji wa simu zenye mfumo wa Android.

 

 

Na Mwandishi Wetu,

MWANDISHI, mshairi, mwanafasihi, mwanasiasa na mchambuzi  mwenye asili ya Uganda na Sudan, Taban Lo Liyong (1936-) alisababisha taharuki katika ulingo wa  usomaji miongo zaidi ya minne iliyopita (mwaka 1969) alipokosoa kwa ukali eneo la Afrika Mashariki aliposema ni ‘jangwa la usomaji’.

Wasomi wa ukanda huo kwa wakati huo walijibu maoni ya msomi huyo gwiji kwa ukali kama vile kummiminia risasi za moto mwilini wakisema kuwa kauli yake ilikuwa ni tusi kwa wasomi wa ukanda huo hususani baada ya kuondokana na ukoloni (walitoa maoni kwamba ilikuwa ni mapema mno kutoa hitimisho hilo lililoonesha kuegemea upande mmoja ikiwa ni takribani miaka kumi tu baada ya nchi za Afrika Mahariki kujipatia uhuru wake).

Kinyume chake leo ikiwa ni miaka 48 tangu Taban atoe maoni hayo, na ikiwa ni  miaka 55 tangu Afrika Mashariki ipate uhuru, mwandishi amethibitisha kile kinachoufanya ukanda huo kujulikana  kama ukanda wenye ‘utamaduni duni wa kusoma’. Kwa kuzungumzia uhalisia, haiwezekani uwepo ‘ustawi ki-uhalisia’ bila kuwapo usomaji wa kuridhisha au kutosha.

Kutokana na hali hiyo, inavutia kuona kuwa  Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Tanzania ikishirikiana na Kampuni ya Jackson Group kulishughulikia  suala  hilo. Ukiwa ni ushirikiano kutoka sekta binafsi na si serikalini, taarifa hiyo inaweza kufungua fursa ya  kuibua mjadala kutoka kada ya wasomi kuhusu ‘ugonjwa wa taaluma’ hususani katika ulingo wa kusoma na au  kukosekana kwake.

Taarifa iliyotolewa na Tigo wiki iliyopita inataarifu wasomaji kwamba kampuni hiyo inashirikiana na Jackson Group kuzindua jukwaa jipya la mtandao linaloitwa Kitabu App ikiwa ni Kitabu elektroniki kilichoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za viatu kwa njia ya sauti na kuona kwa wasomaji tofauti nchini Tanzania.

Jukwaa hilo kama likitumika ipasavyo linaweza kukiteka kizazi cha sasa ambacho ni cha kidijitali na kuibua matumaini ya hamasa kubwa katika kusoma.

Meneja wa Mawasiliano ya Tigo, Woinde Shiasel  anasema Kitabu App inaingia katika soko ikiwa  ni suluhisho si tu kwa wasomaji bali pia kwa waandishi ambao hivi sasa wanaweza kuuza  na kupigia debe mauzo ya vitabu vyao kupitia simu zao za mkononi.

Anasema hiyo itafanikiwa kwa kutumia mtandao wa Tigo 4G LTE.

Ni sahihi kusema  mauzo kwa njia ya mtandao yanaweza kuwa ni mabadiliko katika waandishi kwa kuwa yanaweza kuwafungulia  masoko ya nje.

Shisael anabainisha kuwa  kupitia app hiyo,  inatarajiwa kuwapo mabadiliko katika namna ambavyo Watanzania wanavyouchukulia dhana ya usomaji, dhidi ya kuporomoka kwake ambako kunahusiana na wananchi katika utamaduni duni wa kujisomea hivyo, kuhamasisha  matamanio katika kusoma miongoni mwa jamii na hivyo kuhuisha zoezi hilo lililoporomoka ndani ya nchi.

Anasema; “Hii ni aina ya sauti  ambayo inatakiwa kutoka kwa wahusika wa kitaaluma na mamlaka zinazohusika ikiwa ni kichocheo cha kuibua uchunguzi wa  kitaaluma jambo ambalo ndilo lililokuwa ishara katika miaka ya mwanzo ya 1970 na mwishoni mwa miaka ya 1980 wakati taasisi za  kujifunza  zilipoibuka kikiwa ni kipindi kisichoweza kulinganishwa katika kupanuka kitaaluma.

“Kwa bahati mbaya minara yetu ya taaluma ya kisasa ya vyuo vikuu na mengineyo imekuwa ikijikita katika dhana mbaya ambayo ina imani potofu kwamba lengo la kusoma ni kufaulu katika mitihani tu dhana iliyohodhiwa  na mitazamo  mifupi ambayo haitazami hatima ya mwanafunzi atakapoingia katika maisha ya kiuhalisia ama katika ajira.”

Ukweli unabakia kuwa kulingana na vijana wa Kitanzania, kujisomea si tena kitendo cha thamani kama ilivyokuwa  miaka iliyopita.

Kutokana na mabadiliko ya teknolojia ambako mada nyingi za masomo zinafikiwa kupitia mtandao wa intaneti, ni jambo lisiloepukika kwamba kuna kasi ya mabadiliko kwa kujumuisha  njia za mabadiliko ya kawaida za kupata uelewa kupitia kujifunza kwa kutumia njia ya mtandao.

Jambo linalofikirisha  wengi ukiondoa mtazamo wa zamani kwa wale ambao kitaaluma waliyapitia mambo kabla ya  enzi za kidijitali, ambapo uhalisia ulipozamishwa linaweza kuonekana kama ni kifo cha vitabu ambavyo tulikuwa tunavitumia.

Hata hivyo, Kitabu App  inatoa taswira ya uhamasishaji-waandishi wengi wamekuwa wakiandika kwa lugha ya Kiswahili, ambayo inaeleweka kwa Watanzania walio wengi. Ni uboreshaji wa kweli kutoka Tigo, ambao unafahamika kwa mchango wake katika kuzibadilisha mada za ndani kama Kiswahili kuwapo katika Facebook.

 “Tayari wateja wetu wengi wanapenda kutumia simu kuchati na marafiki  na wanafamila. Kupitia Kitabu App, tunatoa jukwaa la uhakika kwa waandishi, waelekezaji na wasomaji wa jumla sehemu ambayo wanaweza kupata kwa urahisi mada za kusoma kupitia simu ya mkononi,” anasema Shisael.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,922FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles