23.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 26, 2022

Maradona: Wachezaji Argentina hawastahili

MADRID, HISPANIA

MKONGWE wa soka wa timu ya taifa ya Argentina, Diego Maradona, ameweka wazi kuwa, wachezaji wa timu hiyo hawastahili kuvaa jezi za timu ya taifa.

Kauli hiyo ameitoa baada ya kikosi hicho kukubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Venezuela, mchezo wa kirafiki uliopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Hispania.

Mabao ya Salomon Rondon, Jhon Murillo na Josef Martinez yaliweza kuwafanya Venezuela kuibuka na ushindi kwenye Uwanja wa Wanda Metropolitano, huku Argentina ikiwa na nahodha wake, Lionel Messi.

Kutokana na kichapo hicho, Maradona alipoulizwa na waandishi wa habari kwamba, aliionaje timu hiyo? Aliweka wazi kuwa hakuuangalia mchezo huo kwa kuwa anajua uwezo wa wachezaji waliopo.

“Hapana sikuweza kuangalia mchezo wa Argentina, siwezi kuangalia sinema za kutisha. Watu wasio na mamlaka ambao wanatawala timu ya taifa wanadhani walikuwa na uwezo wa kuwafunga Venezuela?

“Ninajisikia vibaya na matokeo ya Argentina na makocha wenzangu pamoja na wachezaji kama vile Ruggeri, Batista, Giusti, Pumpido na Caniggia, lakini ukweli ni kwamba wachezaji wa timu hiyo hawastahili kuvaa jezi ya timu ya taifa,” alisema Maradona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,293FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles