20.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 5, 2022

Takukuru kutaifisha mali za anayetumiwa kutakatisha fedha, kutoroka

Nora Damian, Dar es Salaam

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imetangaza kumtafuta mkazi wa Kinondoni, Magreth Kobelo Bonzaga anayetuhumiwa kutakatisha fedha haramu na kujipatia mali kabla haijazitaifisha.

Akizungumza leo Jumanne Machi 26, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna wa Polisi, Athuman Diwani, amesema wakati uchunguzi ukiendelea mtuhumiwa huyo alitoroka nchini.

Amesema mtuhumiwa huyo kwa kutumia fedha ambazo ni zao la ukwepaji kodi alinunua viwanja vitatu vilivyoko ufukweni katika Manispaa ya Temeke na nyumba tatu za kifahari zilizoko Tegeta Manispaa ya Kinondoni.

“Tumeamua kutangaza kutafutwa kwake kabla ya kutaifisha mali alizojipatia kwa rushwa.

“Asiporudi nchini kwenye kesi inayomkabili madhara yake ni makubwa sana kwake binafsi na familia yake kwa kuwa mali zitataifishwa na kurudishwa serikalini kwa mujibu wa sheria,” amesema Kamishna Diwani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,686FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles