33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Sterling kupewa unahodha England

LONDON, ENGLAND

BAADA ya nyota wa England, Raheem Sterling, kuonesha kiwango cha hali ya juu mwishoni mwa wiki iliyopita katika mchezo wa kuwania kufuzu Euro 2020 dhidi ya Czech Republic, kocha wa timu hiyo, Gareth Southgate, amedai mchezaji huyo ana kila sababu ya kuja kuwa nahodha.

Mchezaji huyo amekuwa kwenye kiwango kizuri ndani ya klabu yake ya Manchester City na ameendelea kufanya hivyo kwa kuifungia England mabao matatu peke yake katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech.

Kocha huyo amedai kwamba, Sterling atakuwa mchezaji mwenye historia kwa kizazi kijacho ambapo kwa sasa amekuwa na kiwango hicho akiwa na umri wa miaka 24.

“Kwa sasa England ina manahodha watatu au wanne na Raheem Sterling ni mmoja kati ya wachezaji ambao wanakuwa kwa ajili ya kuja kuwa kiongozi wa timu kama walivyo wachezaji hao wengine.

“Ukweli ni kwamba, mchezaji huyo ana sifa hizo, lakini si vizuri kuongelea suala hilo la nahodha wakati tayari kikosi kina kiongozi wao, Harry Kane, lakini Sterling kwa kuwa ni ana umri mdogo, ana nafasi kubwa ya kuja kufanya hivyo,” alisema kocha huyo.

Kane ni nahodha namba moja wa kikosi hicho, huku akiwa na wasaidizi wake kama vile Jordan Henderson, Eric Dier, Fabian Delph na Ashley Young, lakini kocha wa timu hiyo anaamini Sterling anaingia kwenye kundi hilo la wachezaji.

Mchezaji huyo hadi sasa amefanikiwa kuwa na mabao 19 msimu huu katika michuano mbalimbali ndani ya klabu yake Manchester City na anatajwa kuingia kwenye orodha ya wachezaji ambao watawania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka endapo ataendelea kuonesha kiwango hicho hadi mwisho wa msimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles