24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mara waanzisha utaratibu wa madaktari bingwa kuzifikia wilaya

Na SHOMARI BINDA


HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Mara imeanzisha huduma ya matibabu ya mkoba kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka hospitali mbalimbali za rufaa nchini.

Huduma hiyo itakuwa ni  kwa kuzitembelea hospitali zote za wilaya kuwatibu wananchi na kuwajengea uwezo wataalamu wa afya kwenye wilaya hizo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara, Dk. Joachim Eyembe  alikuwa akizungumza na waandishi wa habari   baada ya kuanza kutolewa matibabu kwa wananchi wa Wilaya ya Serengeti kutoka kwa madaktari bingwa wa Hospitali ya Rufaa Temeke.

Alisema wameanza na Serengeti na lengo ni kuzifikia hospitali zote za mkoa huo.

Alisema lengo la hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mara licha ya kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi kwa kushirikiana na madaktari kutoka nje ya mkoa lakini wanakwenda kuwajengea uwezo wataalamu wa afya  baada ya hapo waendelee kutoa huduma bora kwa wananchi.

Eyembe alisema Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ndiyo iliyochukua jukumu la kuwagharamia madaktari hao na wananchi wanatibiwa bila kutumia gharama kubwa ambazo wangezitumia kusafiri kuwafuata madaktari bingwa.

Alisema madaktari watano  kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke watasaidia katika kutibu magonjwa ya watoto, wanawake, magonjwa ya kinywa pamoja na wale wanaohitaji upasuaji wa magonjwa mbalimbali.

“Madaktari wamefika Serengeti na tayari wameanza kutoa huduma kwa wananchi ambao wamejitokeza kwa wingi baada ya kupata taarifa ya ujio wa madaktari hawa na kwa kiasi kikubwa watasaidia kutoa huduma.

Daktari bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke Dar es Salaam, Husein Msuma, alisema  wako Mara kutoa huduma kwa wananchi na kushukuru mapokezi waliyoyapata kutoka kwa wenyeji wao.

Alisema kutokana na mapokezi waliyoyapata wanaamini watafanya kazi nzuri na kuwaomba wananchi kujitokeza kupata huduma na kurejea kwenye afya bora na kuendelea kulitumikia taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles