24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Maonyesho ya Vyuo ni tija kwa wananchi katika kukusa elimu ujuzi

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya amevipongeza Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kutoa maarifa mbadala kwa changamoto zinazoikabili jamii nakwamba hatua hiyo inatoa hamasa kwa sababu wanaungana na sera za nchi katika kuongeza fursa za kupata ajira.

Mhadhiri wa Chuo cha Afya Mvumi, John Mpiluka (kulia) akimuelezea Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya shughuli zinazofanywa na chuo cha afya Mvumi katika banda lao la maonesho ya vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanaofanyika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

“Mafunzo ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanagusa eneo muhimu sana la vijana, vijana wengi wamepata elimu hii kwa mafunzo ya muda mfupi miezi mitatu, miezi sita, miaka mitatu ambayo yanawawezesha kupata ujuzi mbalimbali katika utendaji kazi pamoja na kutoa vyeti,” amesema Mmuya.

Mmuya amesema hayo Juni 10, 2022 alipotembelea Maonesho ya Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi yanayofanyika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma ambayo yamesaidia kutoa maarifa kwa wananchi kujua fursa za ajira zilizopo katika maeneo yao, lakini pia kusaidia wataalamu wetu kuwa na maarifa yanayoendana na soko la ajira linalohitajika katika nchini.

Aidha, Mmuya ametoa rai kwa wanavyuo na wakufunzi kuendelea kuangalia mahitaji ya jamii ili waweze kuandaa mafunzo ya muda mfupi ili kuweza kuwapatia wananchi ujuzi unaotakiwa utakaosaidia kuzalisha ajira nyingi.

Nae, Mkurugenzi Mtendaji wa Mitaala na Upimaji, Dk. Annastelllah Sigweyo amesema Baraza inaangalia program zinazoanzisha zainaendana na uhitaji wa jamii baada ya kufanya utafiti wa eneo husika na kwa kuzingatia ushauri wa wadau.

“Tunaangalia uwezo wa chuo kinachotaka kutoa program kama kina uwezo wa kutoa ujuzi husika kwa kuangalia uwezo wa walimu kitaaluma katika kutoa ujuzi, ndipo tunapopitisha mtaala kwa ajili ya chuo husika,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles