25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mangula aendelea kutibiwa Muhimbili

Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Bara, Philip Mangula, anaendelea kutibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), baada ya kuanguka ghafla Februari 28 mwaka huu katika ofisi ndogo za CCM Lumumba mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati Kuu ya CCM.

Februari 29, Rais Dk. John Magufuli alimtembelea Mangula katika hospitali hiyo ili kumjulia hali ambapo alikuwa amelazwa kwenye chumba cha uangalizi maalumu (ICU).

Juzi Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lilieleza kuwa mwili wa Mangula ulikutwa ukiwa na sumu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa, alisema kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama walibaini ndani ya mwili wa Mangula kulipatikana sumu.

“Machi 2 tulipokea taarifa kutoka CCM kuhusu kuwekewa sumu kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Mangula. Katika taarifa hiyo tulielezwa kwamba Mangula alipelekwa Hospitali ya Muhimbili na kulazwa ICU.

“Uchunguzi kuhusu tuhuma ya sumu hiyo ilivyoingia mwilini upelelezi bado unaendelea, Jeshi la Polisi litachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kupanga, kuratibu na kusimamia utekelezaki wa uhalifu hio,” alisema Mambosasa.

Mmoja ya viongozi wa Hospitali ya Tafa Muhimbili, aliiambia MTANZANIA jana kuwa Mangula anaendelea na matibabu hospitalini hapo ingawa anayetakiwa kuzungumzia hali yake kwa undani ni familia yake au Jeshi la Polisi ambalo kwa sasa linaendelea na uchunguzi.

 “Matibabu ya mgonjwa ni ‘privacy’ yake (siri ya mgonjwa) hatuwezi kuzungumzia hilo, nendeni kwenye familia yake mkazungumze nao ndiyo mtapata taarifa zake,” alisema kiongozi huyo aliyekataa kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa suala hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles