27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Polepole ‘atinga’ mahakamani kupeleka faini ya Mashinji

KULWA MZEE – DAR ES SALAAM

Katibu wa itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amewasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kufata utaratibu, wa kulipa faini ya Sh milioni 30 ili kumnusuru DK Vicent Mashinji aliyetiwa hatiani jana.

Polepole amefikia hatua hiyo baada ya Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwatia hatiani viongozi wa Chadema akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe na wenzake wanane.

Mahakama hiyo iliwahukumu kwenda jela kwa kila kosa miezi mitano au kulipa faini jumla Sh milioni 350.

Adhabu hiyo ilitolewa kwa makosa 12 na kosa moja la kula njama washtakiwa wote waliachiwa kwani halikuthibitika.

Akizungumza katika viwanja vya mahakama akiwa ameambatana na wanachama wengine wa chama hicho pamoja na mke wa mfungwa huyo , Polepole amesema amefika kufuata utaratibu ili wamtoe Mashinji.

“Tayari tumeshapewa control namba, tunaenda kulipa kisha tutarudi Mahakama ya Kisutu ili tupewe utaratibu wa kwenda kumtoa gerezani,” amesema Polepole.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,554FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles