22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

MANENO YA MLINGA YAMVURUGA NAIBU WAZIRI

Ramadhan Hassan, Dodoma

Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga(CCM), amemvuruga Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha baada ya kutoa taarifa aliyodai imejaa ukakasi kuliko hoja husika.

Kutokana na hali hiyo Naibu Waziri alimtaka mbunge guyo wakutane nje ya bunge ili amweleze ni nini hasa alikusudia kusema.

Katika mwongozo wake Mkinga aliomba Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kuangalia walimu wa vyuo vikuu ambao wamekuwa wakiomba kufanya mapenzi na wanafunzi wa kike ili wawafaulishe.

Mlinga amedai katika swali la Mbunge wa Mbozi, Paschal Haonga (Chadema), waziri alijibu kwamba kuna wanafunzi wanaonewa kwa kurudishwa madarasa ambapo aliipa taarifa wizara hiyo kuwa tabia hiyo ya kurudisha madarasa wanafunzi kwa kuwaonea ipo vyuo vikuu.

“Dada zetu katika vyuo vikuu wamekuwa walipata adha hiyo na walimu wanajulikana kabisa kuwa huyu ni dume la mbegu, kwa hiyo kama mwanafunzi hatoi hawezi kufaulu na kuna walimu wao wanajulikana kabisa wanataka fedha, naiomba wizara baada ya hii nguvu kuiongeza katika shule za sekondari sasa waelekeze katika vyuo vikuu hasa kwa wanawake ambao wanaonewa,” amesema Mlinga.

Mara baada ya Mlinga kuomba mwongozo, Spika Ndugai alimsimamisha Ole Nasha kutolea ufafanuzi jambo hilo.

“Mheshimiwa Ole Nasha umepokea hii maneno eeeh,” alisema Spika Ndugai.

Akijibu Ole Nasha alisema: “Mheshimiwa Spika nimepokea, isipokuwa maneno aliyotumia Mheshimiwa Mlinga yalinifanya niwe nasikiliza ukakasi zaidi kuliko hoja yake, lakini nitakutana naye nimsikilize hoja yae ilikuwa ipi na alikuwa anataka kusema nini.

“Lakini nitamshauri vile vile mdogo wangu kwamba hili ni Bunge siku nyingine aangalie lugha ambayo anatumia kwa sababu ameongea maneno ambayo si mazuri, lakini hoja yake nitazungumza naye,” amesema Ole Nasha.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles