MAANDAMANO YAWAPONZA SABA ARUSHA

0
820

Janeth Mushi, Arusha

Watu saba wamekamatwa kwa uhamasishaji wa maandamano yasiyo halali, yanayotajwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu.

Watu hao wanadaiwa kuhamasisha maandamano hayo kupitia makundi ya mitandao ya kijamii ya Telegram na Whatsapp.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo, miongoni mwa watuhumiwa hao ni wanafunzi watatu wa vyuo mbalimbali mkoani hapa.

Hata hivyo, Kamanda Ilembo amesuta kutaja majina yao amesema ni kwa sababu za kiupelelezi kwani baadhi yao wameshafikishwa mahakamani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here