27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

SPIKA NDUGAI: MAWAZIRI HAWAZIBWI MDOMO KUMJIBU CAG

Ramadhan Hassan, Dodoma

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema mawaziri hawazibwi midomo kumjibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Spika Ndugai amesema hayo bungeni leo akijibu mwongozo wa Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) ambaye alihoji uhalali wa mawaziri kujibu hoja za CAG.

“Naomba mwongozo wako Mheshimiwa Spika kwa sababu ukiuuliza unaambiwa taarifa zilishatoka inabidi ziende serikalini watafute majibu kwa maana wahusika  waende kwenye zile kamati husika za bunge hili kisha tujadili kama bunge na kutoa maelekezo kwa Serikali na  baadaye tutoe majibu kwa Serikali.

“Lakini mjadala unaoendelea juu ya fedha Trioni 1.5 maana yake ni kama wabunge tumechanganywa utaratibu upi tunatakiwa kuufuata, Mheshimiwa Spika katika kujadili mambo haya ni kwenye taarifa au kila mmoja anasema ya kwake,” amesema.

Akijibu mwongozo huo,Spika Ndugai amesema suala hilo liliishatolewa  ufafanuzi na  Naibu Spika huku akisisitiza mawaziri hawafungwi mdomo kuizungumzia taarifa ya CAG.

“Mimi nadhani hili Mheshimiwa Naibu Spika aliwahi kulitolea ufafanuzi hapa nyuma, maelezo ni hayo hayo hatuwezi kuwafunga mdomo mawaziri kutoa maoni yao hawajasema hapa wamezungumza huko walikozungumza.

“Kwa hiyo wanaendelea tu na utaratibu wetu wa kawaida unaendelea na Mwenyekiti yupo, hakuna tatizo na bunge linaendelea na mchakato wake kama kawaida, anayeamua kuzungumzia azungumzie tu kama kawaida, hakuna shida,” amesema Spika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles