24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mameneja Tanesco kupimwa kwa kigezo kipya

Na Mwandishi wetu-Tabora

NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amewataka mameneja wa Shirika la Umeme, (Tanesco) kuongeza wateja wanaounganishiwa umeme vijijini kwa Sh 27,000 na kwamba hicho ndiyo kitakuwa kigezo cha kupima utendaji wa mameneja hayo katika kanda, mikoa na wilaya.

Mgalu alisema hayo kwa nyakati tofauti, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini, (REA) katika Wilaya za Ulyankhulu, Kaliua, Urambo na Sikonge mkoani Tabora.

Katika Wilaya hizo, Mgalu aliwasha umeme katika makazi ya watu, nyumba za ibada, taasisi za umma, visima vya maji na kuzungumza na wananchi.

Alisema mameneja wa maeneo husika ndiyo wenye dhamana ya kuwafuata wateja katika makazi na kuwashawishi kuunganishiwa umeme badala ya kukaa ofisini na kusubiri wateja.

“Mradi wa REA umekwisha viunganisha na kuwasha umeme katika vijiji vingi, naawaagiza mameneja kufanya kazi ya kuwafuata wananchi huko walipo mkawape elimu ili muwaunganishe na umeme, kwa Sh 27,000, tunataka kuona idadi ya watumiaji umeme inaongezeka,” alisema Mgalu.

Tangu mradi wa REA umeanza wateja 900,000 wameungamishwa na umeme na bado zoezi hilo linaendelea.

Katika ziara yake hiyo, Mgalu alikagua ujenzi wa kituo cha kupokea na kuponza umeme kilichopo katika Kijiji cha Uhuru wilayani Urambo ambapo pamoja na mambo mengine alisema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hicho inayoendelea.

Sambamba na hilo, alikagua eneo ambalo litajengwa kituo kingine cha kupokea na kupoza umeme katika kijiji cha Ipole wilayani Sikonge, ambacho kinatarajia kuanza kujengwa hivi karibuni.

Vituo hivyo vinajengwa mahsusi kwa lengo la kuimarisha upatikani wa umeme mwing na wakutosha  katika Mikoa ya Tabora, Kigoma na pamoja na Katavi,pia mikoa hiyo nayo iunganishwe na gridi ya taifa, na kuacha kutumia umeme unaotokana na mafuta mazito.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles