29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

MAMBO SABA WALIYOKUBALIANA MAWAZIRI WA AFYA AFRIKA MASHARIKI

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini umemalizika leo jijini hapa kwa nchi wanachama kukubaliana maazimio saba ya kuyatekeleza yakiwamo kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na ya mfumo wa hewa.

Akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema makubaliano hayo yamelenga kuimarisha na kuboresha sekta hiyo na afya ya wananchi kwa ujumla.

Aidha, amesema wamekubaliana pia kuongeza uwajibikaji kwenye afya ya mama na mtoto.

“Tumekubaliana kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza tumegundua katika nchi hizo magonjwa yanayoongoza ni pamoja na kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na ya mfumo wa hewa.

“Suala jingine tulilokubaliana ni kutilia mkazo suala la heshima kwa wajawazito, mawaziri wametushauri pia Tanzania kukitambua Chuo cha Upasuaji cha Afrika Mashariki, Kati na Kusini,” amesema.

Waziri Ummy ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, amesema wamkubaliana wamekubaliana pia kuimarisha ushirikiano na ulinzi katika maeneo ya mipaka.

“Kwa sababu nchi zina mipaka lakini magonjwa hayana mipaka tukiimarisha itasaidia kuondoa na kudhibiti uwezekano wa magonjwa hasa ya mlipuko kuenea ikiwemo Zika, Ebola, Dengue, Chikungunya na mengineyo,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amsema pia wamekubaliana kuimarisha masuala ya utawala kwamba kila mmoja ana wajibu kwa nafasi yake kwani sekta ya afya ni mtambuka.

“Tumeona kuna umuhimu mkubwa wa kushirikisha sekta zingine ikiwamo kilimo, maji, elimu, utumishi, mazingira zinahusika kwa ukaribu,” amesema.

Waziri Ummy amesema azimio la saba walilokubaliana katika mkutano huo ni kuweka mkakati wa pamoja kukabiliana na magonjwa akitolea mfano nchi ya Uganda ambao wamepata ugonjwa wa Marbugy unaofanana dalili na ugonjwa wa Ebola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles