29.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

WCB WATOA OFA KWA WASANII WAO

 


NA JESSCA NANGAWE

WAKATI lebo ya WCB ikiwa kwenye hatua za mwisho za ufunguzi wa studio yao mpya ya kisasa, uongozi wa lebo hiyo umetoa ofa kwa wasanii wao wenye kipaji cha utangazaji kujitokeza.

Kiongozi wa lebo hiyo, Nasib Abdul ‘Diamond Platinumz’ amesema, studio hiyo ambayo wamewekeza kiasi kikubwa cha fedha, wataanza na kuangalia na wasanii wake wenye kipaji cha utangazaji.

“Mbali ya kuwa na watangazaji wazoefu, pia fursa tutatoa kwa wasanii wa WCB kutangaza kama wapo ambao wana vipaji tutawapa kipaumbele zaidi,” alisema kiongozi huyo.

Hata hivyo, Diamond aliongeza kwa kusema vijana wajitokeze kuomba nafasi, kwa kuwa ndio walengwa wakuu katika vipindi mbalimbali. Uzinduzi wa studio hiyo unatarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles