24.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

P. DIDDY: SIMU INANIWEKA MBALI NA MUNGU


NEW YORK, MAREKANI

MKONGWE wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Sean Combs, maarufu kwa jina la P.Diddy, amefunguka na kusema matumizi yake ya simu yanamfanya awe mbali na Mungu.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 48, amedai amekuwa akitumia muda mwingi kutumia simu kwa ajili ya mitandao ya kijamii na kusahau kufanya ibada kwa ajili ya Mungu wake.

“Ili kuendana na dunia ya kisasa lazima utakuwa karibu na mitandao ya kijamii, dunia iko mbali sana kwa sasa, hivyo lazima kutumia mitandao mbalimbali kwa ajili ya kujua nini kinaendelea duniani kote.

“Nimekuwa nikitumia muda mwingi kutumia simu yangu na kusahau kufanya ibada kwa ajili ya Mungu wangu, jambo ambalo si zuri,” alisema P.Diddy, wakati anahojiana na mtandao wa GQ, Jumatatu wiki hii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,264FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles